Askofu Mkuu Marek ateuliwa Balozi wa Vatikani nchini Tanzania
BABA Mtakatifu Fransisko amemteua Askofu Mkuu Marek Solczyński kuwa
Balozi mpya wa Vatikani nchini Tanzania. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Mkuu
Solczyński alikuwa Balozi wa Vatikani nchini Georgia, Armenia na Azerbaijan.
Itakumbukwa kwamba, Askofu Mkuu
Solczyński alizaliwa Aprili 7, 1961 huko Stawiszyn, nchini Poland. Baada ya
masomo na majiundo yake ya Kikasisi, mnamo Mei 28, 1987 akapewa Daraja Takatifu
ya Upadri.
Baada ya kufanya utume wake
katika masuala ya diplomasia sehemu mbali mbali, tarehe 26 Novemba 2011, Baba
Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu Mkuu na kumwekwa wakfu
tarehe 6 Januari 2012. Askofu mkuu Marek Solczyński ameshiriki kikamilifu
katika maandalizi ya hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Fransisko nchini Georgia,
Armenia na Azerbaijan aliyoitekeleza mwaka 2016.
Karibu sana Tanzania Baba Marek
ReplyDelete