Askofu Muheria ateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Nyeri, Kenya

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Peter J. Kairo wa Jimbo kuu la Nyeri, Kenya la kung’atuka kutoka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Anthony Muheria kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo kuu la Nyeri, Kenya. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Muheria alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki Kitui na Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki Machakos.
Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Anthony Muheria wa Jimbo kuu la Nyeri, Kenya alizaliwa tarehe 27 Mei 1963 huko Kaburugi. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi kunako tarehe 13 Juni 1993 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, kama Padre wa “Opus Dei”. Tarehe 30 Oktoba 2003 akateuliwa na Papa Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Embu, Kenya na kuwekwa wakfu tarehe 20 Januari 2004. Tarehe 28 Juni 2008 akateuliwa tena na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Kitui, Kenya. Na tarehe 23 Aprili 2017, Baba Mtakatifu Francisko amemteua kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Nyeri, Kenya.
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI