Upotoshaji wa Padri kuoa watolewa ufafanuzi
BAADA ya mitandao ya kijamii pamoja na baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari kupotosha kuwa Kanisa Katoliki limemfungisha ndoa padri wake, imefafanuliwa kuwa, Padri akiomba kuondolewa upadri wake anaruhusiwa kuoa. Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki Bukoba Mhashamu Methodius Kilaini ameeleza kuwa,katika wito wa Upadri katika Kanisa Katoliki , mapadri hawaoi na hiyo ni sheria ama nidhamu ya Kanisa siyo ya Mungu hivyo Papa ana uwezo wa kuitengua. “Katika Kanisa Katoliki Padri ni kasisi, ni kuhani anayetolea sadaka altareni. Kutokana na nidhamu ya Kanisa Padri haruhusiwi kuoa lakini pale anaposhindwa kuendelea na wito wake ama anapoonekana kwamba anashindwa kuuishi upadri wake anaruhusiwa kuomba kuacha na anaruhusiwa kulingana na taratibu za Kanisa. Mapadri ambao mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari vinazungumzia siyo mapadri walishafuata taratibu zote na kupata kibali kutoka kwa Baba Mtakatifu kuwa wamefunguliwa na upadri wao umeondolewa hivyo wana uhuru wa kuoa kwani ...