Mahari yatajwa kuchangia unyanyasaji kijinsia Dodoma

Na Dotto Kwilasa, Dodoma
IMEELEZWA kuwa changamoto ya wazazi kupenda mahari na kuwaoza watoto wao wakiwa wadogo  ni moja ya sababu inayochangia kukithiri kwa ukatili wa kijinsia na mimba za utotoni wilayani Chamwino.
Hayo yameelezwa na baadhi ya viongozi wa vikundi mbalimbali vya uelimishaji rika  kupitia mradi unaosimamiwa na shirika lisilokuwa la kiserikali (WOWAP) chini ya ufadhili wa The faoundation for civil soceity ukiwa na  lengo la kutokomeza ukatili wa kijinsia na mimba za utotono  wilayani humo.
Mmoja wa viongozi hao  wa uelimishaji rika Nyamwanji Nyamwanji akizungumzia suala hilo amesema kuwa ijapokuwa serikali imesema elimu ni bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari lakini jamii bado haioni umuhimu wa elimu na kuthamini mahari na kuoza watoto wao wakiwa wadogo.
Amesema kuwa tatizo lililopo hivi sasa wazazi wengi hawaoni umuhimu wa elimu jambo ambalo inafika wakati hata kuwashawishi watoto wao wafanye vibaya katika mitihani yao ili wasifaulu na baadaye waweze kuwaoza.
“Kwa kweli changamoto ya mahari katika jambo hili tunalopambana nao bado ni kubwa kwani wazazi wengi wanathamini mahari kuliko elimu ya watoto wao wa kike jambo ambalo kwa kweli tunaiomba serikali nayo iliangalie jambo hili kwani watoto wengi wanakatisha masomo.” amesema
Aidha amesema kuwa kwa hali ya sasa wao kama viongozi wa vikundi wamebaini kuwa lipo tatizo la wazazi wengi kutowajibika pia kwa watoto wao katika matumizi ya watoto jambo ambalo nalo linachangioa watoto kujiingiza katika mambo yasiyofaa na kujikuta wakiingia katika vishawishi.
Hata hivyo amesema kuwa lipo tatizo lingine ambalo bado linawakwamisha pindi wanapotaka kushughulikia suala la kutokomeza ukatili huo wa kijinsia na mimba za utotoni nalo ni suala la  kukosa ushirikiano kutoka kwa viongozi wa serikali za vijiji, kata na hata mahakamani.
Amebainisha kuwa suala la rushwa nalo ni kikwazo kwani sheria ingefuatwa na baadhi ya watu wanaowaoa hao watoto au kuwapa mimba wangehukumiwa kwenda jela ingeweza kuwa funzo kwa wengine na kuacha kuwachezea watoto hao wadogo.
Vile vile amesema kuwa changamoto nyingine kwenye jamii ni pamoja na wivu, rushwa, kukosa ushirikiano, waelimishaji kuonekana wabaya kwenye jamii pamoja na kuogopa kutishiwa.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo kutoka WOWAP, Nasra Suleimani amesema kuwa wao kama shirika wanaendelea kuwafuatilia viongozi hao katika kuwakumbusha majukumu yao ya kutoa elimu kwa jamii ili jambo hilo liweze kutokomezwa.
Amesema kuwa wao  kama shirika wanaendea na kuhamasisha jamii kupitia vikundi hivyo kwa njia ya ngoma, wakulima, wafugaji, wasanii lengo likiwa ni kufikia malengo ya suala hilo kuisha kabisa.


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU