Askofu Kinyaia aonya waamini wanaoamini ushirikina

Na Rodrick Minja, Dodoma
ASkofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki  Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaia, amewataka wakristo kuacha tabia ya kukimbilia kwa waganga wa kienyeji wanapopatwa na matatizo mbalimbali ya maisha.
Ameyasema hayo katika Ibada ya Misa Takatifu  alipokuwa anatoa Sakramenti ya Kipaimara kwa vijana 190  katika Parokia ya Mt.Maria Imakulata-Bihawana Jimbo Kuu Katoliki  Dodoma.
Askofu Kinyaia amesema kuwa wakristo wanapaswa kujenga mazoea ya kupeleka matatizo na shida zao kwa Mungu na sio kwa Sangoma yaani waganga wa kienyeji kwani ni kinyume na imani yao.
“Vijana wanaopata Sakramenti ya Kipaimara wanapaswa kuendelea na malezi ya karibu kutoka kwa wazazi na jamii.
Kanisa pia lina jukumu la kutoa malezi endelevu ili kuwasaidia kusimama imara katika imani. Tukizembea hawa ndio watakaokuwa waganga wa kienyeji ama kuamini imani za kishirikina,” amesema Askofu Kinyaia.
Amewaasa vijana hao pamoja na waamini wote kupokea Sakramenti mbalimbali za Kanisa kujitakatifuza na kutumia vipaji vyao kutumikia jamii.
Waamini hao 190 waliopata Sakramenti ya Kipaimara wanatoka katika vigango vigango 13 vya Parokia ya Bihawana.


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU