Ask. Chengula: Wazazi wa mapadri mfahamu upadri si mali

Na Thompson Mpanji, Mbeya
ASKOFU wa Jimbo Katoliki  Mbeya  ametoa wito kwa jamii na wazazi wanakotokea mapadri kuwaombea wapate nguvu za utume badala ya kuwatwika mizigo ya kudai mali.
Askofu Chengula  amesema hayo wakati akitoa   Daraja Takatifu la Upadri kwa Shemasi  Cleophas Sukari katika Kanisa la Hija Parokia ya Mwanjelwa.
Amewasihi wazazi  wanaowatoa watoto wao katika kulitumikia Kanisa kama mapadri kuendelea kuwaombea watoto wao waweze kuishi vyema upadri wao na wamtumikie Mungu ipasavyo.
“Wazazi mvumilie maana watoto wenu wanamtolea Mungu sadaka na kutakatifuza watu. Hawana mali za kuwapa kwani upadri hakuna mali,ni kujitoa kwa Kanisa.
Hakuna mshahara wala posho,wala hakuna madini,kwa hivyo wazazi mnapowatoa watoto wenu  mufahamu kuwa mnayo kazi kubwa ya kuendelea kuwasaidia na kuwalea  kwa ujumla wao,”amesema.
Aidha Askofu Chengula  ametaka mapadri  kufuatilia kwa ukaribu waamini  katika jumuiya zao  kujua changamoto zao za kiimani, wenye shida mbalimbali na kuwasaidia inapowezekana  ili wakue kiimani wasisubiri waamini wawafuate maparokiani.


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU