TAARIFA KWA UMMA


Askofu mteule wa Jimbo Geita Flavian Matindi Kassala sasa atasimikwa rasmi tarehe 12 June 2016 huko Geita Jimboni,TEC imethibitisha.Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Kassala alikuwa ni mkurugenzi wa Kitivo cha "Stella Maris", Mtwara, Chuo kikuu cha Mtakatifu Agostino cha Tanzania. Askofu mteule Kassala alizaliwa tarehe 4 Desemba 1967, Parokia ya Sumve, Jimbo kuu la Mwanza. Alipata masomo yake ya sekondari kutoka Seminari Ndogo ya Mtakatifu Pio wa X, iliyoko Makoko, Jimbo Katoliki la Musoma.
TEC inawatakia maandalizi mema ya kumpokea Baba Askofu Mteule.

Comments

  1. Hongera Kassala, Mungu akupe maisha na utumishi mwema ktk kazi ya Mungu hii, Habby Bugalama LONGO wa zamani Telecentre Sengerema

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU