KILI MARATHON ITUNZE NA KULINDA UUMBAJI-DOKTA AIDAN MSAFIRI



Moja kati ya maeneo yaliyoathirika na mabadiliko ya tabia nchi ni mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro.Ni wazi kuwa nyuzi joto kufikia 35,mvua za kusuasua na maralia za milimani yote haya yamesababishwa na ukataji na uchomaji miti pamoja na shughuli nyingine za kibinadamu.
Na hata katika barua yake,Baba Mtakatifu Papa Francis ameendelea kuikumbusha dunia juu ya wajibu wa wanadamu kutunza na kwa kiwango kikubwa kuuheshimu uumbaji. Katika sura ya tano ya barua ya Papa Francis,ameeleza wazi hatua mbalimbali za kuchukua.Bila kuuheshimu uumbaji hakuna maisha tena.
Mashindano ya Kili Marathoni yenye historia hapa nchini na nje,mwaka huu yameshirikisha wakimbiaji 8,000 wenye sifa kadhaa lakini zaidi wenye imani,wanaoamini uumbaji na wanaomuamini Mwenyezi Mungu.
Naamini kuwa mashindano haya yenye heshima kubwa yanaweza kuwa kielelezo kizuri katika njia  hizi,kuwa chachu ya mshikamano baina ya wanadamu na kuleta amani,kuleta mshikamano na uumbaji katika kulinda na kuheshimu mazingira,mshikamano wa matajiri na masikini katika matumizi sahihi ya rasilimali za dunia hii,mshikamano baina ya imani mbalimbali.
Kielelezo cha Kili Marathoni kina sura hizi,sura ya mlima mrefu ambao katika biblia Takatifu umeelezwa katika Mika 4:2,Isaya 52:7,kumbe wakimbiaji ni vizuri wakazingatia na kutafakari kwa kina juu ya kuuhifadhi mlima Kilimanjaro na mambo ya biblia kiimani.Pia sura ya kukimbia imeashiriwa katika Isaya 40:31,Wakorintho wa kwanza 9:24 na Waebrania 12:1.
Ili kuweza kutunza na kulinda mlima Kilimanjaro na uumbaji wa Mungu kwa ujumla,lazima wanakanisa,serikali na wadau wote waweke dhamira  ya kufufua na kuendeleza,kuziishi tunu kadhaa zikiwemo,kiasi,kujali,kuheshimu,hekima,uwajibikaji,maendeleo endelevu yenye sura ya kibinadamu,mapendo ya kweli kwa Mwenyezi Mungu,wenzetu na uumbaji Mathayo 22:37-39,huruma kwa masikini,rasilimali,ardhi,maji,misitu na rasilimali na vizazi vijavyo.
Kwa ufupi baba Mtakatifu Francis katika barua yake ya kulinda ulimwengu anamwita kila mwanadamu pale alipo kuwa balozi mzuri wa utetezi wa haki za uumbaji na wanadamu kwa ujumla.Elimu kwa watoto na vijana ni kipaumbele ili kufikia lengo la Papa Francis.
Ni vizuri mashindano ya Kili Marathoni ya mwaka ujao 2017 yawe na sura za kiimani na kimaadili pamoja na kuwa na sura za utalii wa kibishara zaidi.Suala la upandaji wa miti 8,000 liwe endelevu pia.
Mwandishi wa makala hii ni balozi wa mabadiliko ya tabia nchi Tanzania.Anapatikana kwa anuani hii S.L.P 3041 Moshi Tanzania.


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU