JARIBIO LA KUMUUA PAPA JOHN PAUL WA PILI LILIVYOSHINDWA

 
MIAKA 35 iliyopita jaribio la kumuua Mtakatifu Papa John Paul II katika eneo la St. Peter's Square lilifanyika
Risasi tatu kutoka kwa kijana Mturuki Mehmet Ali Agca zilimlenga Papa Mei 13 mwaka 1981.
Ali Agca,muuaji mtaalamu alimlenga Papa katika umbali wa karibu sana.Hata hivyo nguvu ya Mungu ilipindisha shabaha yake,risasi moja ikimgusa Papa bega la kulia nyingine ikimpitia katika kidole na tumboni.
Katika kauli yake Papa John Paul II anasema ni mkono wa Mama Bikira Maria uliozuia risasi kumpata sawasawa.
Katika shukrani,Papa alitoa moja ya risasi iliyenga kumtoa uhai kwa Askofu msimamizi wa kaburi la Fatima Ureno.Hadi leo hii risasi hiyi bado ipo katika taji  la sanamu ya Bikira Maria iliyopo katika kaburi hilo





Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU