Watawa waonywa dhidi ya matumizi ya mitandao
Mama Mkuu wa Shirika la Masista
wa Mama Yetu wa Usambara COLU Sista Gaspara Kashamba awataka watawa
wakijiepusha na vitu ambavyo vitavuruga utume wao ikiwepo simu ya mkononi kwani
itawapotosha.
Amesema hayo kwenye Misa
Takatifuikiwa ya kusherekea jubilei ya miaka 50, 25 na kuweka nadhiri za daima
kwa Masista wa Shirika la Mama Yetu wa Usambara (Colu) Kwamndolwa, Korogwe
Jimbo Katoliki Tanga
“Umoja ndiyo msigi wa maisha ya utawa na
kuyafuata yale yashirika ndiyo dira ya kutimiza utume wetu na chamuhimu katika
maisha haya ni kujiepusha na yale ambayo yanawachanganya au kuwafuruga hasa
matumizi ya mitanda ikiwemo simu ya mkononi kwani imeshawapoteza wengi hivyo
masista wangu mjiepushe na hayo,” amesema sista Gaspara
Pia Sista Gaspara ametoa wito kwa
mapadri wote nchini kutambua kuwa kila sista wa shirika COLU ni mwalimu wa dini
mbali na majukumu mengine anaweza kufundisha watu elimu ya dini hivyo wawatumie
ipasavyo katika kueneza injili ya bwana.
Askofu wa Jimbo Katoliki Tanga
Mhashamu Anthony Banzi amewataka watawa kutambua kuwa nadhiri zao walizoziweka
kwa Mungu ziwe ni sala ya kila siku . Masista waliofikia hatua hiyo wajitahidi
kufanyakazi kwa umoja na misingi ya shirika .
Askofu Banzi amewakumbusha
masista waliofikia hatua hiyo kutambua kuwa walitoka mbali, wapo mbali na wanaenda mbali hivyo wanahitaji msaada wa
Mungu kupitia sala zao.
“Sisi tunawaombea kwa Mungu katika yale
mnayosimamia kwani hapo mlipofika mmetoka mbali na mnakwenda mbali na kila mtu
na maisha yake anapaswa kuheshimu nadhiri alizomuwekea Mungu kwa nafasi yake na
iwe sala ya kila siku,” amesema Askofu Banzi
Comments
Post a Comment