Askofu Kinyaiya aonya vijana juu ya mitandao
askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu
Beatus Kinyaiya amewataka wazazi na walezi kuwa na jicho la pekee kwa vijana
wao ambao wanaishi katika kizazi chenye kasi ya maendeleo ya utandawazi.
Akofu Mkuu
Kinyaiya amesema hayo kwenye Ibada ya Misa Takatifu ya Kilele cha Jubilei ya
miaka hamsini tangu kutabarukiwa kwa Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo
Kuu Katoliki Dodoma.
Jubilei
hiyo imeenda sambamba na kutoa Sakramenti ya Kipaimara kwa vijana 75.
Askofu
Kinyaiya amewataka wazazi na walezi kuwasimamia vijana wao vema katika suala la
maadili kwani ulimwengu wa sasa umeghubikwa na utandawazi mkubwa wa teknolojia
ambayo kwao wakiitumia vizuri itawasaidia na wakiitumia vibaya itawapoteza.
“Vijana wa
sasa wanaishi mitandaoni na wanasikia kelele nyingi. Ni vyema wazazi wakendelea
kuwaelekezaa, kuwaonesha mjia sahihi.
Pia
kuwaelekeza kujua namna ya kuchuja sauti mbalimbali za mitandao, kuchuja
mitindo ya maisha ambayo ni kinyume na maadili yetu,” amesema Askofu Mkuu
Kinyaiya.
Pia
amewataka vijana 75 ambao wameimarishwa kwa sakramenti ya Kipaimara kuhakikisha
kuwa wanakuwa askari hodari Yesu Kristo
katika kulitangaza neno la mungu popote pale watakapokuwepo.
Pia
amewataka waimarishwa hao kuhakikisha kuwa wanaisoma biblia ambayo kwayo
itakuwa ni nguzo muhimu ya kuwakuza kiimani na kiroho.
Kwa
nyakati tofauti, Makamu wa Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Padri Chesco
Msaga amesema kuwa dhambi iliingia
ulimwenguni kwa kiburi, kutotii, kutosikiliza sauti ya mwenyezi Mungu na
kutosikiliza maagizo yake mwenyezi Mungu.
Hayo
ameyaeleza alipokuwa akitoa homilia yake katika Ibada ya Misa Takatifu ya
Sikukuu ya Bikira Maria Mkingiwa wa Dhambi ya Asili,ibada iliyokwenda sambamba
na wanovisi 10 wa Shirika la Upendo wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili na
kuweka nadhiri za kwanza ndani ya shirika hilo.
Amewaasa
wanovisi hao ambao wameweka nadhiri za kwanza za utawa kuwa Mungu amewaita kuishi maisha ya useja,
na kuweka nadhiri ya ufukara hivyo hawatajilimbikizia mali bali watatumia vyote
kwa sifa na utukufu wa mwenyezi Mungu.
Wanovisi walioweka nadhiri za kwanza ni Agatha Urassa,
Alice Kamwara, Editha Yunde, Felista Laurenti, Jonisia Munyi, Mary Okello,
Moureen Ogwaro, Veneranda Sangawe, Victoria Richard pamoja na Winny Francis.
Comments
Post a Comment