Polisi wajipanga kudhibiti uhalifu msimu wa Krismas
Kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka
Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam limeimarisha ulinzi katika
maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam,hususani katika taasisi mbalimbali za
fedha (benki),maduka ya kubadilishia Fedha za kigeni na sehemu zenye mkusanyiko
wa maduka mengi .
Akizungumza na wandishi wa habari
Jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam SACP
Lazaro Mambosasa amesema kuwa kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka
kumekuwa na baadhi ya watu ambao hujitafutia kipato kisicho cha halali kwa
kufanya vitendo vya kiuhalifu,hivyo kutokana na hali hiyo jeshi la Polisi Kanda
maalumu limejipanga kikamilifu kuhakikisha kwamba hakuna tukio lolote la
uhalifu litakalojitokeza.
Kamanda Mambosasa alizidi
kuongezea kwa kuwataka wanachi wasiwe na hofu pindi watakapoona idadi kubwa ya Askari wakifanya doria katika
maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam
na badala yake watoe ushirikiano kwa kutoa taaarifa za wahalifu.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi
Kanda maalumu ya Dar es Salaam wamefanikiwa kukamata vipande 20 vya meno ya
tembo vyenye thamani ya milion 87.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu
Lazaro Mambosasa amebainisha kuwa, awali walipokea taarifa kuwa kuna watu
wanaojihusha na biashara hiyo ya nyara za serikali,ndipo polisi waliweka mtego
na kufanikiwa kukamata watuhumiwa watatu wakiwa na vipande hivyo,watuhumiwa ho
wanaendelea kuhojiwa kwakushirikiana na maofisa wa maliasili na utalii na
upelelezi ukikamilika watapelekwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Comments
Post a Comment