Maisha ya mtawa ni kusali-Askofu Msonganzila asema
Askofu wa Jimbo Katoliki Musoma MichaeL Msonganzila amewakumbusha
watawa kuwa watu wa sala, ili kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu kama wito wao
unavyotaka.
Askofu Msonganzila ameyasema hayo Desemba 8 mwaka
huu, wakati wa Misa Takatifu ya kuweka nadhiri za kwanza, za daima na jubilei
ya miaka 25 na 50, kwa masista wa shirika la Moyo safi wa Maria Afrika katika Kanisa la Novisiati lilopo
Makoko,Jimboni humo.
“Msiache kumbipu Mungu kupitia sala, yeye yupo
kila sehemu ukimbipu tu anajipu wakati huo huo au anaweza kuchelewa kidogo
kukujibu kwani hujibu kwa wakati.
Maisha yenu ya utawa yanahitaji
majitoleo ya sala, kuwaombea watu, kuiombea dunia na kujiombea ninyi
wenyewe,”amesema Askofu Msonganzila.
Amewaomba wazazi pia kuwaombea
watawa wote wa kike na wa kiuume ,ili kupata nguvu katika wito wao,kwa kuwa
peke yao hawawezi .
Mama Mkuu wa shirika hilo Sista
Maria Lucy Magumba amewashukuru Masista hao kwa kuamua kumutumikia Mungu katika
maisha yao yote, licha ya changamoto mbalimbali walizokumbana nazo katika
maisha ya utawa,na hata wale walioweka nadhili za kwanza kwa kuamua kumtumikia
Mungu katika maisha yao.
Comments
Post a Comment