Walei ni uhai wa Kanisa-Askofu Ruzoka
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki
Tabora Mhashamu Paul Ruzoka
amewakumbusha walei kuchukua nafasi yao katika Kanisa bila kusahau wajibu wao
wa kutakatifuza malimwengu bila kusita kwani ni wajibu wao.
Rai hiyo
ameitoa hivi karibuni alipokuwa akitoa mahubiri yake katika kanisa la kiaskofu
la Mtakatifu Terezia wa Mtoto Yesu Tabora na kuhimiza waaamini kukimbia dhambi
na kuishi maisha yanayompendeza Mungu wakiwa bado hapa duniani.
Akitoa
mahubiri yake Askofu Mkuu Ruzoka amesema Mtaguso wa Vaticano wa mwaka 1965
ulioweka wazi nafasi ya walei kuwa ni moja ya nguzo muhimu katika uhai wa
Kanisa,”Walei ni wengi, wana nguvu na wanapatikana katika kila sehemu kama
vile, mitaani, vijijini, vigangoni , maeneo ya kazi, na hata maeneo ya biashara wakitumika vizuri wana nguvu kubwa
ya kueneza Imani Katoliki,” Askofu Mkuu Ruzoka amesema.
Aidha
amesisitiza umuhimu wa familia zote kuishi Imani Katoliki na kudumisha maadili
katika ndoa zao ili kupata mapadri na
watawa wenye kupeleka sura ya Kristo Yesu kwa watu.
Pia amewaomba
mapadri kuonesha umuhimu wa huduma ya
padri katika Kanisa, kwani bila mapari Imani Katoliki iko mashakani, na hivyo
kutoa wito kwa mapadri wote kuhudumia waamini kwa moyo wa upendo na furaha.
Mapadri ndio
wanao walisha watu Neno la Mungu na Sakramenti za Kanisa, hivyo wazazi wote
hawana budi kulea miito mitakatifu katika famili zao. Katika Adhimisho hilo la Misa Takatifu
Jubilei ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Idara ya Halmashauri walei
ilizinduliwa.
Katika
sherehe hiyo ya Familia kijimbo, madekano wa dekania zote tatu walitoa taarifa
ya michango ya kutegemeza ofisi ya Askofu na kupokelewa.Aidha katika Misa hiyo,
Askofu Mkuu Ruzoka aliwaalika waamini wote kumshukuru Mungu kwa kutimiza miaka
90 kijimbo tangu kupatikana kwa mapadre watatu wanajimbo, yaani Padre .Philipo
Luziga, Padre Simoni Makulumo, na Padre Raphael Kavula ambao wote ni Marehemu.
Akimalizia
mahubiri yake , Askofu Mkuu Ruzoka amewaalika mapadri, watawa na waamini wote
kutolea sala zao na kumuombea aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Mbeya marehemu Askofu Evarist Chengula
pumziko la milele.
Comments
Post a Comment