Kadinali Pengo asisitiza umuhimu wa Ekaristi Takatifu
ASkofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mwadhama Polycarp
Kardinali Pengo amefungua rasmi Kanisa dogo la kuabudia Ekaristi Takatifu
katika Parokia ya Mt. Fransisko wa Sales Mkuza na kuwataka waamini kutambua
umuhimu wa Ekaristi Takatifu katika maisha yao.
Katika
uzinduzi wa Kanisa hilo Kardinali Pengo amesema Kanisa hilo la kuabudia Mungu
daima linaweza kuonekana dogo katika macho ya waamini lakini licha ya udogo
wake ndimo chemchemi ya upendo, huruma ya kimungu ilipo.
Hivyo kila
mkristo akitambua umuhimu wa Ekaristi Takatifu maishani mwake atafika kunako
kanisa hilo muda wote kusema na Yesu wa Ekaristi.
“Leo
tunaiweka parokia yetu katika historia ya Mungu kwa upendo wake kwetu sisi
wanadamun na tunafuraha kubwa ya kubariki na kufungua kanisa dogo kwa ajili ya
kuabudia Mungu wa daima, hivyo sote tutambue thamani ya Ekaristi Takatifu
katikati ya maisha yetu kama alivyosema Baba Mt. Yohana II,” amesema.
Aidha
Kardinali Pengo ametumia kuzindua kitabu cha MUNGU NI MUWEZA WA YOTE
kilichoandikwa na muumini wa Parokia ya Mkuza Ndugu Mathias Tiyabiyona
aliyetembea takribani siku 32 kwa miguu kuelekea Butiama kwenye Kaburi la Baba
wa Taifa Julius Kambarage Nyerere akiwa na sanamu ya Mama Bikira Maria, na
lengo la safari hiyo lilikuwa kumtangaza mama Bikira Maria.
Muamini
huyo huyo ameliambia gazeti kiongozi kuwa kabla ya safari hiyo aliyoianza
August 4, 2014 hadi Septemba 2, 2014 akiwa kwenye sala ya Rozari Takatifu
aliijiwa na sauti masikioni mwake ikimwambia ya kuwa watu wan chi hii ya
Tanzania hawajui kuwa mimi ni mwombezi wao, ikiwa ni sauti ya Mama Bikira
Maria.
Baada ya
uzinduzi huo Kadinali Pengo alielekea kwenye Jubilei ya miaka 50 ya Parokia ya
Chalinze. Parokia ya Mt. Fransisko wa Sales Mkuza inaongozwa na paroko Pius
Thomas wa Shirika la Mt. Fransisko wa Sales
Comments
Post a Comment