Posts
Showing posts from January, 2018
Papa Francisko: Shikamaneni ili kupambana na balaa la njaa Barani Afrika
- Get link
- X
- Other Apps
Familia ya Mungu Barani Afrika hauna budi kuungana, kushikamana na kushirikiana kwa dhati ili kupambana na balaa la njaa na utapiamlo wa kutisha miongoni mwa watoto unaoendelea kudhalilisha utu na heshima ya binadamu kwa sehemu kubwa ya Bara la Afrika. Hiki ni kiini cha ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, kwenda kwa Rais Alpha Condè, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika wakati huu ambapo, Umoja wa Afrika unafanya kikao chake cha thelathini kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO. Baba Mtakatifu anaunga mkono jitihada za utekelezaji wa Azimio la Malabo lililotiwa sahihi kunako mwaka 2014 huko Malabo, Equatorial New Guinea, ambapo Umoja wa Afrika (AU), uliziagiza nchi wanachama kutenga angalau asilimia 10% ya bajeti kwa ajili ya sekta ya kilimo. Mkwamo wa utekelezaji yakinifu wa Azimio la MAPUTO la mwaka 2003 na baadaye MALABO, 2014 katika nchi nyingi za Kiafrika, kumetajwa...
BENKI YA BIASHARA YA MKOMBOZI YAPATA MKURUGENZI MTENDAJI MPYA
- Get link
- X
- Other Apps
Januari 27, 2018: Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Biashara Mkombozi imetangaza uteuzi wa Bw. George Shumbusho kama Mkurugenzi Mtendaji mpya wa benki hiyo kuanzia Disemba 1, 2017. Uteuzi huu unafuatia kustaafu kwa Mama Edwina Lupembe ambaye ni miongoni mwa viongozi maarufu katika sekta ya kibenki na ameiongoza benki ya Mkombozi kwa miaka tisa. Akizungumza katika hafla maalumu ya kumuaga Mama Lupembe na kumkaribisha mkurugenzi mpya, katika Baraza la Maaskofu Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Bw. Method Kashonda aliwashukuru wote wawili kwa makabidhiano mazuri ya ofisi ambayo yameleta imani kuwa benki inabaki katika mikono salama. Mwenyekiti huyo alimpongeza Mama Lupembe kwa umahiri wake katika uongozi. Mama Lupembe alijiunga na benki hiyo Agosti 29, 2009 huku akiwa ameshika nafasi za juu kwa zaidi ya miaka 20 katika sekta ya kibenki, taasisi za umma na kuwa mjumbe katika bodi mbalimbali za mashirika ya umma na binafsi. ...