Posts

Showing posts from December, 2018

TAARIFA

Image

Askofu Nyaisonga atuma salamu za Noeli Mwaka Mpya

Image
+   Asema Noeli ni uhai si mauaji ya watu na mazingira +   Aitaka serikali kuboresha huduma ya afya nchini   Na Suzan Kaneka- Mpanda R ais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Askofu Gervas Nyaisonga ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki Mpanda amewata wananchi wote nchini Tanzania kutunza mazingira. Ameyasema hayo mapema hii leo wakati akitoa salamu ya sikukuu za  Krismas na mwaka mpya 2019 ambapo amesema kuwa sherehe hizi zinatukumbusha kuyaishi mafumbo ya kuzaliwa kwawetu Yesu Kristo, kuzaliwa upya na kupata uzima mpya. “Noeli ni sikukuu ya kuadhimisha uhai kwa kuuthamini kuulinda, kuutetea na kuuheshimu uhai wa mwanadamu hivyo tuadhimishe sikukuu ya Noeli kwa kuyarudia maagano yetu” amesema Baba Askofu Nyaisonga amesema  kuwa uhai unategemea mazingira mazuri yanayomuwezesha binadamu kuishi, hivyo amewataka waumini kutunza mazingira , kuyalinda mazingira kuwa kutokata miti hovyo, kutoharibu vyanzo vya maji kwa k...

Fahamu ukweli kuhusu elimu ya nyota na utabiri, chuma ulete

Image
J E, unazungumzaje kuhusu “chumaulete” ambapo inasemekana pesa za mtu mmoja zinaweza kwenda kwa mwingine kwa kufanya ushirikina? Jibu: Habari za “chumaulete” ni uongo wa kifukara. Ni uongo ambao kudhihirika kwake lazima ufikiri wa kinyume. Waafrika, katika dhiki zetu na ufukara wetu huwa na hadithi za kupata mali au pesa “kwa che”. Ndiyo kisa, kati yetu hustawi habari za kupata mali kwa uchawi au ushirikina, au kwa kutumia mapepo (yaani mashetani), au kwa kutumia majini, au kwa kupitia Frimasoni na kadhalika. Kila mara tuna maelezo ya ajabu kwa wanaokuwa matajiri kati yetu, yaani usiwe na nyumba au gari kuwazidi walio wengi mhali ulipo. Wengine tutasema ni wachawi. Wengine tutasema wanatumia mapepo au “majini” kama Waislamu waaminivyo. Wengine tutasema wanapata kwa kuwa ni wanachama wa Frimasoni na kadhalika. Kifupi, hatukosi maelezo sisi! Kumbe, kwa sababu ya dhiki zetu, Waafrika huwa tunaaminishana kwamba kuna njia za mikato za kupatia pesa au utajiri. Hiyo ndiyo imani in...

Ushoga siyo haki ni udhalilishaji wa binadamu

Image
Na Pascal Mwanache, Dar es salaam K atika kuadhimisha miaka 70 ya azimio la ulimwengu la haki za binadamu viongozi wa dini kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) wamekutana na kuweka wazi kuwa wanalo jukumu la kusimamia haki huku wakibainisha kuwa vitendo vya ushoga vinadhalilisha utu wa mwanadamu. Akitoa mada katika kongamano hilo Katibu Mkuu wa TEC Padri Dkt. Charles Kitima amesema kuwa katika jamii zote, haki za binadamu zipo hasa katika mila na desturi na kwamba haki za msingi ni stahili za kila binadamu kwa sababu ya utu wake. “Maandiko Matakatifu yanatambua haki za binadamu kwa mfano haki ya kuwa na familia, kuoa na kuolewa. Ndiyo maana ushoga unapigwa vita. Ndoa iwe na fursa ya kuendeleza ubinadamu. Utaletaje ndoa ambayo haina ya kuzaa” amehoji Padri Kitima. Aidha amesema kuwa viongozi wa dini hawana budi kupigania na kusimamia haki za wanyonge kama ambavyo wanaendelea kuf...