Ask. Chengula azikwa Mbeya
Na Pascal Mwanache, Mbeya W AZIRI wa Fedha na Mipango nchini Dkt. Philip Mpango amesema kuwa ni jukumu la viongozi wa dini kukemea uovu uliopo katika jamii na hata viongozi wa serikali wanaposhindwa kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia watanzania. Ameeleza hayo katika Misa Takatifu ya maziko ya marehemu Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo Katoliki Mbeya iliyofanyika kwenye Kanisa la Hija Parokia ya Mwanjelwa, ambapo Dkt. Mpango amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Ponge Magufuli. Dkt. Mpango amesema kuwa marehemu Askofu Chengula alikuwa na uthubutu wa kukemea uovu katika jamii ya Tanzania, jambo ambalo viongozi wa dini hawana budi kuliendeleza. Amebainisha kuwa Askofu Chengula alikuwa ni kiongozi wa mfano kwa waamini wa Mbeya na watu wote. “Waamini wa Jimbo Katoliki la Mbeya na wanachi wa Mbeya Mungu aliwapa zawadi kubwa, aliyoihamisha kutoka Iringa akawaleteeni ninyi. Huyu alikuwa ni kiongozi wa mfano. Aliwaelekeza watu kwa Mungu. Alithamini...