Papa: Wanawake Mapadri Kanisa Katoliki hapana

Asisitiza Karismatiki kufwata taratibu za Kanisa Katoliki

Vatikani

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani Papa Fransisko amesema, Kanisa Katoliki halitaruhusu kuwa na wanawake mapadri ijapokuwa linaheshimu nafasi ya wanawake katika maendeleo ya Kanisa.

Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara wake nchini Swedeni, Novemba 1, 2016.

Katika msafara huo Papa Fransisko alizungumzia kuhusu Wakimbizi na wahamiaji; Daraja Takatifu ya Upadri kwa wanawake na msimamo wa Kanisa Katoliki; Majadiliano ya kiekumene na Kanisa la Kiorthodox, Kanisa Anglikani na Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Duniani; Amani, upatanisho na umoja wa kitaifa nchini Venezuela.

Pia amezungumzia Changamoto ya ukanimungu Barani Ulaya; biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo .

Baba Mtakatifu amewashukuru na kuwapongeza waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara wake kwa kazi nyeti waliyoifanya wakati wa Sala na ushuhuda wa kiekumene kati ya Waluteri na Wakatoliki.

Baba Mtakatifu ametumia fursa hiyo, kuwashukuru wananchi wa Swedeni ambao wamekuwa na utamaduni wa upendo na ukarimu kwa wakimbizi na wahamiaji, kiasi kwamba, takwimu zinaonesha kwamba. Nchini humo kuna wakimbizi na wahamiaji wapatao millioni 9 na wengi wao wanatarajiwa kupewa uraia wa Sweden.

Wanawake mapadri hapana
Baba Mtakatifu anasema, msimamo wa Kanisa Katoliki kuhusu Daraja Takatifu ya Upadri kwa wanawake, ulikwisha kutolewa na Mtakatifu Yohane Paulo II na hakuna mabadiliko yoyote juu ya hilo.

Kuhusu uwezo wa wanawake katika kutekeleza dhamana na wajibu wao kama Mapadri na Maaskofu, anasema, hana uhakika na mchuano mkali kati ya wanawake mapadre na wanaume mapadri!

Wanawake wana karama na mapaji ambayo wakiyatumia vyema na kwa uaminifu wanaweza kufanya vyema zaidi hata kuliko wanaume.

Haya ni mambo ambayo yanaweza kuchambuliwa katika nyaraka mbali mbali za maisha na utume wa Kanisa.
Mtakatifu Petro ni mkuu wa kikosi kizima cha Mitume waliokabidhiwa dhamana ya kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu hadi miisho ya dunia.
Mwelekeo wa Bikira Maria ni ushuhuda wa dhamana na utume wa wanawake katika ustawi na maendeleo ya Kanisa la Kristo. Wakati wa Pentekoste, Bikira Maria alikuwa pamoja na Mitume wa Yesu.

Kanisa ni Mama na mwalimu na hakuna Kanisa bila ya kuwa na mwelekeo huu wa Kimama! Wanawake wana nafasi kubwa katika kuliendeleza Kanisa kutokana na karama na nafasi zao lakini si lazima wawe mapadri kwani hata Kristo hakuchagua mitume 12 wanawake.

Ekumene
Baba Mtakatifu anasema, Mwaka 2016 umefunikwa na matukio mengi ya majadiliano ya kiekumene kati ya Kanisa Katoliki, Kanisa la Kiorthodox, Kanisa la Kianglikani pamoja na Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Duniani. Ni matumaini yake kwamba, ataendelea kushiriki kikamilifu katika mchakato wa majadiliano ya kiekumene yanayosimikwa katika uhalisia wa maisha ya waamini kama alivyofanya alipowatembelea waamini wa Kanisa la Kipentekosti mjini Caserta, nchini Italia. Kanisa Katoliki kwa miaka mingi halikuwatendea haki waamini wa Makanisa ya Kipentekosti, kumbe, hapa kuna haja ya kuomba msamaha na kuanza mchakato wa kuganga na kuponya madonda ya utengano, chuki na uhasama kati ya waamini. Baba Mtakatifu anasema, anapenda kuendeleza mchakato wa majadiliano ya kiekumene kwani ni sehemu ya vinasaba vya maisha na utume wake. Majadiliano katika maisha ni chachu muhimu sana inayoweza kudumisha majadiliano katika ngazi mbali mbali ili kujenga utamaduni wa kufahamiana, kuheshimiana na kuthaminiana kama ndugu wamoja katika Kristo Yesu.

Azungumzia kuhusu Karesmatiki

Chama cha Kikatoliki cha Uhamsho wa Roho Mtakatifu kwa kushirikiana na Chama cha Wakarisimatiki Wakatoliki kunako Mwaka 2017 wanaadhimisha Jubilei ya miaka 50 ya uwepo na utume wao ndani ya Kanisa; matunda ya maadhimisho ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatikani. Vyama hivi wakati wa Mkesha wa Pentekosti vitafanya kongamano la kimataifa naye anatarajiwa kushiriki kikamilifu.
Baba Mtakatifu anawataka waandishi wa habari kuwa makini na matumizi ya Neno “Pentekosti” kwani linaweza kuleta utata kidogo!

Baba Mtakatifu anasema, Chama cha Wakarisimatiki Wakatoliki kilipoanzishwa nchini Argentina, alikuwa wa kwanza kukipinga kwamba, alitamani kuona Liturujia ikiheshimiwa na wala si kugeuka kuwa ni shule na mahali ambapo waamini walikuwa wanaendesha ibada zao kama makanisa ya kipentekosti!
Lakini leo hii, anamang’amuzi na mwelekeo na mtazamo tofauti kabisa, kwani taratibu aliweza kugundua tunu bora katika maisha na utume wa Wakarisimatiki Wakatoliki kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Kanisa la Kristo LAKINI KWA KUFWATA TARATIBU ZA KANISA KATOLIKI.

Kuhusu wakimbizi na wahamiaji
Baba Mtakatifu anakaza kusema, kuna haja ya kutofautisha kati ya wakimbizi na wahamiaji. Wakimbizi ni watu wanaolazimika kuzikimbia nchi zao kwa sababu mbali mbali na wanayo haki ya kimataifa inayowalinda na kuwasimamia ili waweze kupata hifadhi na usalama wa maisha yao.
Ni watu wanaokimbia vita, dhuluma na nyanyaso; baa la njaa na majanga asilia yanayotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Wakimbizi wanahitaji msaada, huduma na fursa za ajira. Nchini Sweden, wakimbizi wamepewa kipaumbele cha pekee na Serikali katika kuwasaidia kujifunza, utamaduni na mapokeo ya wananchi wa Sweden.

Baba Mtakatifu anakumbusha kwamba, Bara la Ulaya limejengeka kutokana na watu kutoka katika makabila, lugha na tamaduni mbali mbali.

Anasikitika kuona kwamba, kuna baadhi ya nchi za Ulaya zinazojikita katika sera ya uchoyo kwa kutaka kufunga mipaka ya nchi zao, badala ya kuwa wazi na wakarimu kwa kubainisha sera na miakati ya kuwapokea na kuwapatia hifadhi bora ya maisha. Kila nchi iwajibike kadiri ya uwezo na rasilimali iliyopo. Wakimbizi na wahamiaji wasipopata hifadhi, wanatumbukizwa katika utumwa mamboleo na matokeo yake hata utamaduni unadumaa kutokana na woga na hofu isiyokuwa na mashiko!


Hapa Baba Mtakatifu anawataka wakuu wa nchi kujivika fadhila ya busara, ili kuhakikisha kwamba, wakimbizi na wahamiaji wanapata fursa ya watoto wao kwenda shule, kupata matibabu msingi, makazi bora na salama pamoja na fursa ya kazi. Sweden ni mfano bora wa kuigwa katika kuwapokea, kuwahifadhi na kuwahudumia wakimbizi na wahamiaji.

Comments

  1. To be frank it is much better for the christian community + other communities vatcan II number 322-326 by Aloisius Daniel Babati Manyara

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU