Ask. Ngalalekumtwa: Haki na amani vitawale

ASKOFU wa Jimbo Katoliki Iringa, Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa ameongoza maelfu ya waamini wa jimbo hilo kufunga kilele cha Mwaka wa Yubilei ya huruma ya Mungu huku akisisitiza kuwa haki na amani havina budi kutawala kwa watu wote.
Askofu Ngalalekumtwa amesema kwamba waamini wanaagizwa kuhurumia maudhi waliyotendewa na wenzao na pia kushiriki shida za wenzo ziwe za kimwili au kiroho.
“Katekesi ya Kanisa Katoliki inahamasisha kwamba kuwa na matendo ya huruma, mintaarafu mwili ni kama kulisha wenye njaa, wenye kiu, kuwavisha wasio na nguo, kuwakaribisha wageni, kutembelea wagonjwa,kuwaokoa waliotekwa na kuzikwa wakfu. Matendo ya kiroho ni pamoja na kuwafunza wasiojua neno la Mungu, kuwashauri wenye mashaka, kuwaonya wadhambi, kuvumilia mabaya” ameeleza

Maadhimisho ya kufunga kwa mwaka wa huruma yalitanguliwa na maandamano yaliyohusisha mapadri, watawa wa kike na kiume pamoja na waamini kutoka parokia 37 zilizopo jimboni Iringa yakianzia katika Kanisa la Bikira Maria Consolta, Parokia ya Mshindo, kupitia barabara ya Uhindini, Soko Kuu na baadae barabara ya Dodoma hadi viwanja vya Kichangani Senta ya Vijana Parokia ya Kihesa.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU