Tanzania yachukua hatua kukabiliana na nzige
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, amesema Tanzania inashiriki kusaidia kupoteza nzige
walioibuka na kushambulia mashamba nchini Kenya ili wasiongezeke tatizo likawa
kubwa zaidi lakini pia lisije likahamia nchini Tanzania.
Majaliwa alisema hayo bungeni jijini Dodoma eo
Alhamisi Januari 30, alipokuwa kijibu swali la Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato
Chumi aliyetaka kujua namna serikali ilivyojipanga kukabiliana na wadudu hao.
“Hili baa la nzige ambalo tayari limeshafika
katika baadhi ya nchi jirani hasa za Afrika Mashariki, nilikuwa napenda
kufahamu, serikali imejipangaje katika kukabiliana na kudhibiti masuala haya?”
amehoji.
Akijibu swali hilo, Majaliwa amesema kuhusu
nzige ambao jirani zetu mazao yao yanaharibiwa, ni wadudu hatari ambao
wakiingia nchini watamaliza mazao yetu hivyo serikali imemechukua tahadhari
ambapo Wizara ya Kilimo inaendelea kuwasiliana na Wizara ya Kilimo nchini Kenya
kuona mwenendo na ukuaji wa tatizo hilo.
“Na sisi huku tunajipanga kwa namna ambavyo
tunaweza kushiriki kikamilifu lakini serikali yetu inashiriki pia kusaidia
nchini kwenye kupoteza wadudu hao ili wasiongezeke tatizo likawa kubwa nchini
Kenya lakini pia lisije likahamia nchini kwetu.
“Sasa bado nitoe wito kwa mikoa na wilaya na
vijiji vilivyoko mipakani kuwa makini na hao wadudu nzige pale ambapo watawaona
wakiingia watoe taarifa haraka sana kwenye mamlaka zao ili hatua kamili
zichukliwe,: amesema.
Pamoja na mambo mengine, amesisiza kuwa serikali
imejipanga kudhibiti hali hiyo na itendelea kudhibiti hali hiyo ili Tanzania
isije kupata tatizo hilo.
Comments
Post a Comment