Papa Francisko alitaka Kanisa kulinda na kutetea uhai
Baba Mtakatifu
Francisko, Jumatano tarehe 12 Juni 2019 kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la
Mtakatifu Petro mjini Vatican, baada ya Katekesi kuhusu Safari ya Injili
Ulimwenguni mintarafu Kitabu cha Matendo ya Mitume, amewaambia waamini na
mahujaji waliofurika kwa wingi mjini Vatican kwamba, Kanisa limezaliwa kutoka
katika nguvu ya Fumbo la Ufufuko. Mwanga wa Kristo Mfufuka katika Jumuiya ya
kwanza ya Wafuasi wa Kristo umevunjilia mbali ubinafsi na woga dhidi ya wafuasi
wengine. Mwanga huu ukawahamasisha kuwa ni vyombo na mashuhuda wa ujenzi wa
Kanisa hadi miisho ya dunia! Huko, wakatangaza na kushuhudia upendo wa Mungu
uliomwilishwa katika umoja na ushirikiano; ushuhuda na udugu! Hii ni changamoto
kwa Wakristo kuendelea kuishi katika umoja unaofumbatwa katika utofauti wao
kama ulivyoshuhudiwa na Kristo Yesu.
Baba Mtakatifu anaendelea kuwakumbusha
waamini kwamba, maisha ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kama waamini
wanaitwa na kuhamasishwa kulinda, kuitunza na kuidumisha, tangu pale mtoto
anapotungwa mimba tumboni mwa mama yake, hadi mauti yanapomfika kadiri ya
mpango wa Mungu, hata pale watu wanapokumbana na magonjwa pamoja na mahangaiko
mbali mbali ya maisha. Hakuna mwenye haki ya “kufyekelea mbali zawadi ya maisha
ya binadamu”. Baba Mtakatifu anawaalika waamini kuendelea kusimama kidete, ili
kuhakikisha kwamba, uhai wa binadamu unaheshimiwa na kuthaminiwa na kwa njia
hii, kuwekza kutangaza na kushuhudi tunu msingi za maisha ya Kikristo katika
mazingira ya kifamilia. Baba Mtakatifu amehitimisha Katekesi yake kwa kusema
kwamba, Sherehe ya Pentekoste inafunga rasmi shamara shamra za Sherehe ya
Pentekoste.
Comments
Post a Comment