Ask. Minde: Watoto wanaopelekwa seminari waandaliwe kiroho
Askofu
wa Jimbo Katoliki Kahama Mhashamu Ludovick Minde ALCO/OSS ametoa wito kwa
wazazi na walezi kuwa wanapaswa
kuwaandaa kiroho na malezi ya wito watoto wanaowapeleka kujiunga na seminari.
Wito huo ameutoa wakati wa Misa Takatifu ya
Sherehe ya Seminari ndogo ya Malkia wa Mitume, Ushirombo iliyoambatana na ufunguzi wa Bwalo la kulia
chakula la seminari hiyo.
Askofu Minde amesema katika mambo ya Mungu
yanapaswa kuongozwa na Roho Mtakatifu kuanzia kwenye familia.
Familia zidumu katika maisha ya uongofu,
sala na kuwaandaa watoto kwa miitombalimbali ukiwemo wito wa upadri hata kabla
hawajajiunga na seminari.
“Tusifanye mambo peke yetu tumuombe Mungu atuongoze katika maisha na mipango yetu
kwa kufaata mafundisho ya Kanisa.
“Tunapoandaa
mambo yetu tusiongozwe na jazba
hatuwezi kuwa na mafanikio mazuri kwenye maisha yetu kama hatumshirikishi
Mungu,” amesema Askofu Minde.
Amewataka waamini kuomba hekima
ya Mungu kwa moyo wa sala amabazo zitafanikisha mipango yao.
Askofu Minde amesema kuwa, Seminari ya Malikia wa Mitume iliyopo
katika Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima , Ushirombo ilikuwa inakabiliwa
na sehemu ya kulia chakula kwa sasa kukamilika kwa bwalo hilo kumewaondolea
adha hiyo waseminari hao.
Aidha katika misa hiyo kulifanyika harambee
ya kuchangia seminari hiyo na jumla ya sh milioni 26.1 zilipatikana ambapo
askofu Minde amewashukuru wazazi na walezi kwa kupeleka watoto wao kusoma hapo
na kuwapongeza waamini wote waliojitoa kuchangia.
Comments
Post a Comment