Msimamo wa Magufuli kuhusu uzazi wa mpango wapongezwa
Na Pascal Mwanache, Dar M SIMAMO alioutoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli juu ya uzazi wa mpango umepongezwa kwa kuwa kukithiri kwa vitendo vya matumizi ya vidhibiti mimba kumeharibu taifa na kushambulia maadili, utamaduni na imani ya taifa huku dhana hizo zikiwa ni itikadi ovu za magharibi za kudhibiti ukuaji wa idadi ya watu. Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Uhai nchini (Pro life) Emil Hagamu katika tathmini yake ambapo amesema kuwa watu wa Ulaya wamepita katika miongo mbalimbali, imefikia mahali wameharibikiwa hivyo mawazo na itikadi zao ovu ndizo zinazoletwa kwetu Afrika hasa Tanzania. “Hiki ndicho Nyerere alichosema, alisema ili tuendelee tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Kwa hiyo watu ndiyo namba moja. Asikudanganye mtu, nchi zote za Ulaya zilipata maendeleo kwa sababu kuu tatu: Walitunyonya kiuchumi na kisiasa, biashara ya utumwa ambapo walihitaji watu, na idadi yao ni kubwa. Uki promote co...