‘Ukristo ni vita’ Ask. Amani
Na Erick Paschal, Moshi WAKRISTO wakatoliki nchini wametakiwa kutambua kuwa ukristo ni vita na mapambano ambapo maisha ya hapa duniani ni ya muda kwa ajili ya kujiandaa na maisha ya milele. Rai hiyo imetolewa na Askofu Mkuu Isaac Amani wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha wakati akitoa homilia yake kwenye adhimisho la Misa Takatifu ya kilele cha Jubilei ya miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania Bara kanda ya kaskazini, Misa iliyoambatana na sherehe ya Bikira Maria mpalizwa mbinguni. Askofu Amani amesema kuwa mpango wa Mungu mara zote ni kumuokoa mwanadamu, na maovu anayoyatenda mwanadamu yanakwenda kinyume na mpango wa Mungu, kwa kuwa Mungu anashughulikia wokovu kwa sababu binadamu ana thamani mbele yake. Askofu Amani amesisitiza kuwa kila mwanadamu hana budi kujitathmini na kujichunguza kwani mpango wa Mungu siku zote ni wokovu hivyo kila mmoja ana wajibu wa kujiuliza kama ni wakala wa Mungu ama wa shetani kwa matendo. Vijana ni zamu yenu kuwa wamisionari Wakati huo huo vijana n...