Baba Mtakatifu Francisko kupitia Wosia wake wa Kitume Amoris laetitia , yaani Furaha ya Upendo ndani ya familia , anaonesha kuheshimu na kujali changamoto ambazo familia zote wanakumbana nazo kwa namna moja au nyingine. Kardinali Lorenzo Baldisseri, katibu mkuu wa Sinodi za Maaskofu amesema kuwa, Wosia huo wa kitume umefika kwa wakati muafaka ambapo familia zimo kwenye kinzani kubwa kihistoria. Kinzani kutambua wajihi wake, kujitambua kijinsia mwanamke na mwanaume, kuheshimu tunu ya ndoa na familia, kutunza uhai na haki msingi za watoto na kila mwana familia, kujaliana na kupendana kwa furaha. Wosia wa kitume, Amoris laetitia , unaeleza kwamba ni ngumu kuwatia moyo wana ndoa kuhusu uaminifu na kujitoa kwa kila mmoja bila kutia cheche hija ya kukua, kukomaa na kuzama katika upendo kati ya wana ndoa na ndani ya wanafamilia wote. Kwa sababu upendo ndio chemichemi na msingi wa ndoa, na upendo huo katika kukua na kukomaa kwake unarutubika na kupanuka kwa kuzaa na kulea watoto, na kuw...