“Majimbo yote yawe na tovuti”
KURUGENZI ya Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) imeshauriwa kuhimiza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika majimbo yote ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi na kupanua wigo wa Mawasiliano. Akizungumza na wakurugenzi wa Mawasiliano Jamii kutoka baadhi ya majimbo Katoliki Tanzania katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) kwenye Semina juu ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), pia mbinu za Mawasiliano, Mratibu wa Mawasiliano Jamii wa Umoja wa Wanachama Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) Padri Chrisantus Ndaga amesema Kanisa Katoliki bado lina changamoto katika matumizi ya mitandao ya kijamii hususani tovuti za majimbo. Padri Ndaga ameyashauri majimbo yote Katoliki nchini Tanzania kufungua tovuti na mitandao mingine ya kijamii ili kutanua wigo wa Mawasiliano ndani na nje ya majimbo wakati akiwahimiza wakurugenzi wa Idara za Mawasiliano Jamii majimboni kuwaendeleza kitaaluma wa...