Posts

Wazazi waaswa kusaidia Utoto Mtakatifu kuinjilisha

Image
      WAZAZI na walezi kote nchini wametakiwa kujitoa kwa kila hali na mali kuwasaidia watoto kushiriki matamasha ya kiroho, kongamano na hija   za Utoto Mtakatifu, ikiwa ni sehemu ya malezi kwa mtoto.       Akitoa homilia katika Misa Takatifu kigango cha Mbutu Parokia ya Kimbiji Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Paroko Msaidizi wa Parokia hiyo Padri Justus Lugayimkam amewakumbusha na kuwataka wazazi na walezi wote kutambua kuwa, jukumu   la kulea Watoto wa Utoto Mtakatifu, lipo mikononi mwao na mtoto anapokua katika malezi ya dini humfanya awe mwenye heshima na mchamungu.           Amesema wapo walezi ambao jukumu la Utoto Mtakatifu wamewaachia walimu jambo linaloleta ugumu kwa walimu   pindi   inapotokea watoto wanahitaji kushiriki katika matamasha mbalimbali . “Watoto wanahitaji mchango wa kifedha ili waweze kushiriki matamasha na watoto wenzao kutoka katika map...

‘Kipaumbele cha Padri ni Ekaristi Takatifu’

PAROKO wa Parokia ya Isimani Padri Leornad Maliva amewaasa mapadri kuangalia vipaumbele vya utume wao hasa wanapopangiwa maeneo mapya ya kazi. Padri Maliva ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Mapdri Jimbo Katoliki   Iringa (UMWAI) amesema, suala la msingi kwa padri yeyote anapopangiwa eneo jipya la uchungaji ni uwepo wa Ekaristi Takatifu na sio umeme, barabara ya lami na mitandao ya simu. Padri ahakikishe kuwa katika ratiba yake ya kila siku anapanga muda wa kukaa na Yesu wa Ekaristi Takatifu. “Padri hana sababu yeyote inayomfanya akose muda wa kuabudu Ekaristi kila siku. Padre ni mwadhimishaji wa Ekaristi Takatifu na ni vema aiabudu hata baada ya misa. Katika sakramenti ya Ekaristi Takatifu, Yesu ametuachia ukumbusho wa mateso yake ili mateso na mahangaiko yetu yapate faraja katika kuiabudu hiyo Ekaristi. Kwa padri, kuabudu Ekaristi takatifu ni kielelezo cha unyenyekevu wa kukubali kuwa padre ni kiumbe dhaifu anayepata na kuchota nguvu za utume wake katika ukumbush...

Majadiliano ya kiekumene hayakwepeki: Askofu Ruzoka asisitiza

JIMBO Kuu Katoliki Tabora linaendeleza mchakato wa majadiliano ya kiekumene ili kujenga na kudumisha majadiliano ya kiekumene miongoni mwa Wakristo. Askofu Mkuu Paul Ruzoka wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora, katika mahojiano na gazeti hili hivi karibuni amesema kuwa,   majadiliano ya kiekumene ndani ya Kanisa ni kati ya mada zilizojadiliwa na kutolewa maamuzi na Sinodi ya kwanza ya Jimbo Kuu Tabora iliyoadhimishwa hivi karibuni kwa kuongozwa na kauli mbiu “Yesu hu seba” yaani “Yesu ni taa ya uhai wa   imani yetu.” Kanisa linatambua kwamba, Kristo Yesu ndiye muasisi wake na kwamba, aliunda: Kanisa moja, Takatifu, Katoliki na la Mitume. Kumbe, majadiliano ya kiekumene miongoni mwa Makanisa ni jitihada za kutaka kujenga na kudumisha umoja wa Kanisa kama Kristo mwenyewe alivyoliombea, liwe na umoja. (Rej. Yn. 17: 21) Ikumbukwe kwamba, asili ya Kanisa ni moja,”ameeleza Askofu Mkuu Ruzoka, Aidha amesisitiza kuwa, Maaskofu Mahalia kwa kushirikiana na Khalifa wa Mtakatifu Petr...

Askofu Minde azidua Jubilei ya miaka 100 ya Upadri Kahama

Image
ASKOFU LUDOVICK Minde wa jimbo la Kahama amezindua rasmi Jubilee ya miaka 100   ya padri na kutoa wito kwa   mapadri kuupenda na kuuenzi   upadri wao ambao ni zawadi kutoka kwa Mungu. Akihubiri   katika Misa Takatifu ya uzinduzi wa Jubilei hiyo iliyofanyika   hivi karibuni katika Kanisa Kuu la jimbo la Mtakatifu Karoli Lwanga Parokia ya Kahama mjini Askofu Minde amewasisitiza mapadri   kuutunza upadri kama lulu   uweze   kuonekana   katika utume wao kwa Kanisa. Aidha amewakubusha mapadri wajibu wao na kuwataka   kuendelea kuomba neema   hiyo   ya kuupenda   zaidi upadri , kuuenzi   kwa sababu ni zawadi   kuu ya   milele toka   kwa   Mungu   aliyowajalia   ndani ya kanisa kwa kushirikishwa ukuhani huo. “Mapadri wanahitaji kuombewa katika utume wao ili waweze kung’aa   kama mwanga   katika   dunia hii   katika   utumishi wao   wa uijilishaji ...

Mapadri msiogope kusema na kusimamia ukweli -Askofu Niwemugizi

Image
“DAIMA msiogope kuusema ukweli ambao utawaweka watu wa Mungu huru na kutoka katika mwenendo mbaya usiompendeza Mungu.” Askofu Severine NiweMugizi wa Jimbo Katoliki Rulenge Ngara   ametoa mwito huo kwa mapadri wakati wa Misa maalumu ya kutoa Daraja Takatifu la Ushemasi kwa Shemasi Alex Blandi. Akiwatia moyo Mapadri, Askofu Niwe-Mugizi amesema kuwa, msemakweli daima maisha yake yako hatarini lakini wajue utume wao wameukabidhi mikononi mwa Mungu ambaye atawaongoza na kuwavusha kwa kila vikwazo hasa vitokanavyo na kusema ukweli. "Mpendwa Shemasi Alex na Mapadri kuweni wajasiri kwa kusema ukweli. Najua kuna watu wasiopenda kuusikia ukweli na mkweli daima huchukiwa na maisha yake yamo hatarini, yawekeni maisha yenu mikononi mwa Mungu matahifadhiwa naye," amesema. Aliwahimiza mapadri daima kuwa wavumulivu, wenye subira, wenye kusamehe wasiokata tamaa . Pia   kuwa wabunifu kwa kuwa na muda wa kusema na muda wa kunyamaza. Aidha Askofu Niwemugizi alielezea hal...