UTOAJI MIMBA, VIDHIBITI MIMBA TISHIO NCHINI

n Na Pascal Mwanache, Dar

IMEELEZWA kuwa utoaji wa mimba na matumizi ya vidhibiti mimba ni dhana zinazolenga kuharibu taifa na kushambulia maadili, utamaduni na imani ya taifa huku dhana hizo zikiwa ni itikadi ovu za magharibi za kudhibiti ukuaji wa idadi ya watu.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Uhai nchini (Pro life) Emil Hagamu katika tathmini yake ambapo amesema kuwa utoaji wa mimba na matumizi ya vidhibiti mimba ni vitu vigeni kwa waafrika na ili vikubalike hutumika kampeni na propaganda yenye maneno mazuri ili kuficha uovu uliomo ndani yake.
“Taifa lolote linaweza kuangamizwa njia ya vita. Vita kubwa tunayopigwa watanzania ni mashambulizi dhidi ya maadili ya Taifa ambayo ndiyo yanayotafsiri jamii ilivyo. Ukiua utamaduni unaojenga misingi ya maadili na imani utakua umeua taifa. Na ukitaka kuua vizuri Taifa basi lenga kwa vijana, ukibomoa misingi ya hawa lazima utamomonyoa taifa”
Aidha amesema kuwa fikra za kuzaa, idadi ya watoto, na namna ya kupishana kwa watoto ni sehemu ya mila na desturi za watu husika, ambapo tangu mwanzo mwanadamu amekuwa na uelekeo wa kupenda kuzaa watoto wengi.
Ameongeza kuwa Afrika inaongoza kwa kuwa na desturi ya kupenda na kuthamini uhai wa mwanadamu ndiyo maana watoto ni kitu cha thamani sana katika jamii zao.
“Watu wa Ulaya wamepita katika miongo mbalimbali, imefikia mahali wameharibikiwa. Hivyo mawazo na itikadi zao ovu ndizo zinazoletwa kwetu Afrika hasa Tanzania. Wanaleta kampeni za kudhibiti ukuaji wa idadi ya watu kwa kuweka matumizi ya vidhibiti mimba na utoaji mimba. Wanatumia maneno mazuri kama afya ya uzazi, yaani wanaangalia uzazi kama kitu kinachoharibu afya” amesisitiza.
Amesema kuwa ni uongo mkubwa kusema uzazi wa mpango unapunguza mimba zisizotarajiwa, na kusema kuwa uzazi wa mpango unachochea mimba zisizotarajiwa, akitolea mfano wa nchi ya Marekani ambako kuna kiwango cha udhibiti mimba kwa asilimia 80 lakini bado kuna sheria za utoaji mimba zimetungwa.
“Wanasema vidhibiti mimba vinasaidia kupunguza vifo vya kina mama na watoto, hii siyo kweli. Kinachosaidia kupunguza vifo vya kina mama na watoto ni mipango mizuri, utashi wa kisiasa na huduma bora za afya. Ni kuelimisha wahudumu, kuwa na vifaa vya kutosha na wataalamu, kutoa huduma kwa uzalendo ili mhudumiwa aone kuwa sehemu ya huduma ni sehemu salama na siyo sehemu ya kifo” ameongeza.
Ameeleza kuwa dawa zinazotumika kudhibiti mimba zinageuza uzazi kuwa ugonjwa na mtoto anayepatikana na uzazi kuwa balaa, huku akitahadharisha kuwa kiwango cha wanawake wanaoshindwa kupata mimba kinaongezeka ikiwa ni madhara ya matumizi ya dawa hizo. 
Pia amesema hiyo inaashiria kuwa kwa sasa uwezekano wa wasichana kuolewa ni mdogo kuliko ilivyokuwa zamani, na kubainisha kuwa asilimia 25 ya wasichana wanaotumia vidhibiti mimba chini ya umri wa miaka 25 wanapata saratani ya matiti.
Katika hatua nyingine Ndugu Hagamu ametahadharisha kuwa kuna sera zinazotekelezwa na serikali na washirika wengine juu ya afya ya uzazi ambazo zinaweza kuliangamiza taifa, kwani walengwa wa sera hizo ni vijana kuanzia miaka 15, ambapo amesema kuwa umri huo siyo sahihi kuwachanganyia mitaala ya mahusiano.
“Mtoto hastahili kuzaa wala kupanga uzazi kwani kwa umri huu anastahili kuwa shuleni. Huu ni umri wa makuzi na malezi na kwa kuwa hajafikisha miaka 18 anakuwa yupo chini ya uangalizi wa wazazi. Sasa inastaajabisha, eti watoto wa miaka 15 wanawekwa kwenye kampeni za kuwafundisha afya ya uzazi ikiwa ni pamoja na haki ya kuwa huru katika kufanya maamuzi ya mahusiano na jinsia. Wanafundishwa shuleni na vyuoni mambo haya, na wanayaita afya ya uzazi kwa vijana. Hili taifa linakwenda wapi?” amehoji.


Comments

  1. Ameeleza kuwa dawa zinazotumika kudhibiti mimba zinageuza uzazi https://digg.com/u/tuvanphathai kwani walengwa wa sera hizo ni vijana kuanzia miaka 15, ambapo amesema kuwa umri huo siyo sahihi kuwachanganyia mitaala

    ReplyDelete
  2. Kutoka Bila Matumaini Hadi Kufurahi Kupita Kiasi - Dk. Dawn Aliwezesha Iwezekane!”

    "Nilipopoteza kabisa tumaini la kuwa mama, ulimwengu wangu ulijihisi tupu. Nilijaribu kila kitu, lakini hakuna kitu kilichofanya kazi, na nilivunjika moyo. Kisha nikampata Dk. Dawn, na kila kitu kilibadilika. Kwa uchawi wake wenye nguvu wa ujauzito na mwongozo, ndoto zangu zilitimia—sasa nimebarikiwa kupata watoto wawili warembo! Leo, mimi na mume wangu ndio wenzi wenye furaha zaidi ulimwenguni. Maneno hayawezi kueleza jinsi ninavyoshukuru kwa kurudia maisha yetu ya Dawn."

    Wasiliana na tabia yake ya ujauzito,
    Tahajia ya mapenzi/ tahajia ya kufunga/ tahajia ya kuokoa/
    Spell kuponya magonjwa na magonjwa na zaidi:


    Nambari ya WhatsApp: +2349046229159

    Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete
  3. Sikuwahi kuamini kitu kama hiki kingeweza kunitokea hadi ndoa yangu ilipokaribia kuisha kabisa.

    Mume wangu alibadilika ghafla. Mwanaume ambaye hapo awali alinipenda na kunijali akawa baridi, asiyejali, na mwenye hasira bila sababu. Aliacha kuonyesha nia katika ndoa yetu, akaniepuka kabisa, na hatimaye akaniomba talaka. Nilivunjika moyo kwa sababu nilimpenda mume wangu kwa moyo wangu wote.
    Mambo yalizidi kuwa mabaya aliponizuia kila mahali — WhatsApp, Facebook, Instagram — kana kwamba sijawahi kuwepo. Nililia kila usiku nikijiuliza nilifanya nini kibaya.
    Siku moja, rafiki wa karibu alinitembelea na kunitambulisha kwa mtu wa kiroho anayeitwa Dkt. Dawn. Kwa kweli, mwanzoni nilikuwa na shaka, lakini niliamua kumweleza kila kitu kwa sababu sikuwa na chochote cha kupoteza.

    Dkt. Dawn alinisomea mambo ya kiroho, na nilishtuka. Alifichua siri kuhusu ndoa yangu na maisha yangu binafsi ambayo hakuna mtu aliyejua. Kila kitu alichosema kilikuwa sahihi 100%. Kisha akafichua kwamba mwanamke mwingine alikuwa amemloga mume wangu. Mwanamke huyu alikuwa akimtembelea mara nyingi, na kwa upumbavu niliamini ilikuwa kuhusu kazi tu.
    Dkt. Dawn alinisaidia kuvunja uchawi na akafanya ibada yenye nguvu ya kurejesha upendo kwa ndoa yangu.
    Kwa mshangao wangu mkubwa, muda mfupi tu baadaye, mume wangu alinifungulia kizuizi mwenyewe na kuanza kunipigia simu na kunitumia ujumbe mwingi, akiniomba nimsamehe na nirudi nyumbani. Mwanzoni nilimpuuza kwa sababu ya maumivu aliyonisababishia, lakini hatimaye alirudi nyumbani akiwa na zawadi na machozi machoni mwake akiomba nafasi nyingine.
    Leo, ndoa yetu ni imara zaidi, yenye furaha zaidi, na yenye amani zaidi kuliko hapo awali. Mapenzi kati yetu yanahisi upya kabisa.
    Kana kwamba hiyo haitoshi, Dkt. Dawn baadaye alinisaidia na ibada ya ujauzito kwa sababu tulikuwa tumejitahidi kwa miaka mingi kupata watoto. Ndani ya wiki 8, nilipata mimba kiasili, na leo tumebarikiwa na wavulana wawili wazuri wenye afya njema.
    Nitaendelea kushukuru milele.
    Ukihitaji: Uchawi wa mapenzi wa kuungana tena na mpenzi wako wa zamani
    . Usaidizi wa kurejesha ndoa
    . Tamaduni za ujauzito za kupata mimba
    . Usaidizi wa kiroho kwa kesi za mahakamani au kupona urithi
    . Mwongozo na ulinzi wa kiroho
    Ninapendekeza sana Dkt. Dawn. Ushuhuda wangu ni wa kweli, na furaha yangu leo ni uthibitisho. WhatsApp yake: +2349046229159. dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI