MADHARA YA TETEMEKO BUKOBA:KANISA KATOLIKI LAATHIRIKA, MISAADA YAHITAJIKA

Sarah Pelaji, Dar es Salaam

BAADA ya tetemeko la ardhi kuukumba mkoa wa Kagera, Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki Bukoba Mhashamu Methodius Kilaini ameeleza kuwa, Kanisa Katoliki limepata maafa na hasara ikiwemo kuharibika kwa nyumba ya Askofu wa Jimbo hilo, Mhashamu Desiderius Romwa, nyumba yake anayoishi, makanisa, shule zinazomilikiwa na Kanisa, Chuo Kikuu (SAUT) tawi la Bukoba na nyumba za mapadri.

“Kwakweli si Kanisa tu lililopata maafa bali jamii nzima. Nyumba nyingi zimeanguka, watu analala nje, hawana makazi, wamefariki na kupata majeruhi.

Kwa upande wa Kanisa hali ni mbaya maana Kanisa la kwanza kujengwa katika Mkoa wa Kagera la Kashozi ambalo lilijengwa mwaka 1892-1897 limepata nyufa amabzo zinaweza kusababisha Kanisa hilo likaanguka. Nyuma ya Askofu wa Jimbo huko Ntungamo nayo imapata nyufa hadi amahamia kwenye kichumba ambacho kwakweli anajisitiri tu.

Mimi mwenyewe nimehama kwenye nyumba yangu ya kuishi kwani imepata nyufa na vitu vimeharibika hapafai kuishi. Nyumaba ya mapadri huko kashozi nayo imaharibika haifai kuishi mtu hivyo mapadri wanalala nje kwenye magari,” ameeleza Askofu Kilaini.

Amezitaja baadhi ya shule za Kanisa Katoliki zilizoharibika kuwa ni pamoja na shule ya wasichana ya Hekima ambapo mabweni yameanguka, shule ya Ihungo iliyojengwa mwaka 1949 nayo imaharibika na kanisa lake limebomoka na nyumba ya mapadri.

Akizungumzia namna ya kusaidia maafa hayo Askofu Kilaini amesema kuwa, kila Askofu anajaribu kuweka mikakati ya namna anavyoweza kusaidia maafa hayo ili kufanikisha lile linalowezekana kwa sasa.

“Kwa upande wa jimbo la Bukoba tunaanza kuangalia kanisa la Kashozi ambalo linaweza kuanguka  wakati wowote . Tunataka kukarabati ili lisianguke na kufanya juhudi mapadri wa Kashozi na Ihungo wapate pa kulala".

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU