Huwezi kutenganisha utume wa walei na maendeleo ya Kanisa- Kard.Pengo asema
IMEELEZWA kuwa waamini walei nchini wamekuwa chachu ya maendeleo ya Kanisa kwa ushiriki wao kikamilifu katika mipango na utekelezaji wake katika hatua mbalimbali. Hayo yameelezwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya jubilei ya miaka 50 ya utume wa walei Tanzania, yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Msimbazi Center jijini Dar es salaam na kufikia kilele chake Juni 16, 2019. Kardinali Pengo ameeleza kuwa walei hawapaswi kujiona kuwa ni watu wa kuambiwa tu kana kwamba hawana mchango wowote, bali wanapaswa kuona kuwa wao ni sehemu muhimu ya maendeleo ya Kanisa. “Kabla ya Mtaguso Mkuu wa pili wa Vatikani waamini walei walisubiri watekelezewe kila kitu kana kwamba hawana chochote cha kutoa. Baada ya mtaguso huo Kanisa limetambua nafasi ya walei na hivyo ni lazima wajue kuwa wana sehemu muhimu ya kufanya, siyo tu kulipa zaka na kusikiliza maelekezo” ameeleza Kardi...