PAPA AMEMTEUA PADRI ANTHONY LAGWEN KUWA ASKOFU WA MBULU
Mh. Pd. Anthony Lagwen ateuliwa kuwa Askofu Jimbo Katoliki la Mbulu Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Anthony Lagwen kutoka Jimbo Katoliki la Mbulu, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Mbulu, nchini Tanzania. Askofu mteule Anthony Lagwen alizaliwa tarehe 5 Julai 1967 huko Tlawi, Jimboni Mbulu. Baada ya masomo yake ya msingi, alibahatika kuendelea na masomo ya sekondari katika Seminari Ndogo ya Sanu, Jimbo Katoliki la Mbulu. Akapata masomo ya falsafa kutoka Seminari kuu ya Ntungamo, iliyoko Jimbo Katoliki la Bukoba na baadaye akahamia Seminari kuu ya Kipalapala, Jimbo kuu la Tabora ili kuendelea na masomo ya kitaalimungu. Tarehe 18 Oktoba 1999 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo Katoliki Mbulu. Tangu wakati huo, katika maisha na utume wake wa Kipadre kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2000, alikuwa Paroko-usu wa Parokia ya Bashay. Kati ya mwaka 2000 hadi mwaka 2004 akepelekwa na Jimbo kujiendeleza zaidi katika masuala ya biashara kwenye Chuo Kikuu cha Mtaka...