KUELEKEA MAHAFALI YA 19: SAUT YAJIVUNIA ELIMU BORA
CHUO KIKUU cha Mtakatifu Agustino (SAUT) cha jijini Mwanza kimeendelea kusifiwa kwa kutoa elimu bora hasa kwa njia ya vitendo kwa wananchi ndani na nje ya Tanzania. Hayo yamebainika zikiwa zimesalia siku chache kabla ya chuo hicho kusherehekea mahafali yake ya 19 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1998. Afisa Uhusiano wa chuo hicho Living Komu akizungumza na gazeti la Kiongozi amesema kuwa SAUT ni chuo cha kujivunia kwa wanafunzi wote waliopita hapo kwa maana ni chuo kitoacho wanafunzi bora kitaaluma na kimaadili. ‘Ili uweze kutambulika na kuheshimiwa ni lazima uwe na nidhamu njema na pia taaluma iliyotukuka, hivyo kama chuo kinajitahidi na kimeweza kufanya kadri ya uwezo wake kuzalisha wanafunzi wenye vigezo bora vya kuuzika katika soko la ajira ya sasa na hata baadaye ndani na nje ya Tanzania,’ amesema Komu. Amewakumbusha wanafunzi wote ambao wanakwenda kuhitimu katika mahafali ya 19 kuwa ni vyema watumie elimu na nidhamu waliyofunzwa hapo chuoni na kuwa kioo kizuri ka...