Padri Makunde Katibu Mkuu mpya wa AMECEA

Maaskofu wanaounda Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki nchi za Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) wamemteua Padri Antoni Makunde wa Jimbo Katoliki la Mbeya kuwa Katibu Mkuu mpya wa shirikisho hilo.

Uteuzi huo umekuja kufuatia uchaguzi uliofanyika katika kuhitimishwa kwa Mkutano Mkuu wa 19 wa AMECEA Agusti 21, 2018  Addis Ababa.

Uteuzi huo umetangazwa na Mwenyekiti wa AMECEA anayemaliza muda wake Mwadhama
 Berhaneyesus Kardinali Souraphiel, Askofu Mkuu wa Addis Ababa katika misa ya kufungwa kwa mkutano huo.

Padri Makunde anachukua nafasi kutoka kwa Padri Ferdinand Lugonzo wa Jimbo Katoliki
Kakamega nchini Kenya aliyehudumu kwa vipindi viwili katika nafasi hiyo.

Aidha Mwadhama Berhaneyesus ametangaza uteuzi wa Padri Stephen Mbugua, kutoka Jimbo Katoliki Nakuru nchini Kenya kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Cha Afrika Mashariki– CUEA.


Padri Mbugua anachukua nafasi ya Justus Mbae, kutoka Kenya ambaye amemaliza kipindi chake cha kutumikia kama Makamu Mkuu wa Chuo.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU