MBINGA: WATANZANIA WATAKIWA KUDUMISHA TUNU ZA UMOJA NA AMANI


 
                                         
Watanzania wameshauriwa kudumisha umoja na mshikamano uliopo ili tunu ya amani iliyopo katika nchi iweze kudumu. Hayo yamesemwa hivi karibuni  na Padre Christian Mhagama wakati akihubiri katika misa takatifu ya jubilee ya mapadri 11 wa jimbo la Mbinga katika kanisa kuu la Mtakatifu Kilian jimboni Mbinga.
Padre Christian amesema kuwa,” haitoshi kuimba tu kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani pasipo kuienzi mifumo ya umoja na mshikamano iliyowekwa na waasisi wetu.” Amesema migogoro iliyopo kati ya wakulima na wafugaji  inaashiria kupoteza tunu hiyo ya amani na kuiweka Tanzania kuonekana kwa ndani  kuwa sio kisiwa cha amani.
Aidha  amewataka mapadri hao kumi na moja {11} kuulinda umoja walioudhamiria kuufuata katika kauli mbiu yao waliyoichagua wakati walipopata upadri.  Amesema mapadri hao katika sherehe yao ya upadri waliandika maneno  “Kwa kuwa mkate ni mmoja sisi tuliowengi tu mwili mmoja kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja”
Padri Christian amefafanua kuwa, kauli mbiu hiyo ni ya watu wote na mataifa yote. Amesema Bwana wetu Yesu Kristo alijihusisha sana na kuwafanya watu wote wawe pamoja . Kazi yake ilikuwa kubomoa ukuta au utengano uliopo kati ya watu waliotengana kimila na kidesturi,alibomoa ukuta kati ya wayahudi na wasamalia  na watu wa mataifa mengine kuwa kitu kimoja. Amesema Yesu aliondoa pia utengano uliokuwepo kati ya wanaume na wanawake.
Ameelezea kuwa, mapadri hao walifanya vema kuchukua maneno yenye dhamira ya kuwataka kuwa kitu kimoja,  Amesema “idadi hiyo ya mapadri 11 inawakilisha idadi ya mitume 11, kasoro mmoja ambaye ni Yuda Iskarioti.  Amesema kama wangekuwa 12  leo tungemtafuta msaliti”,
Naye naibu waziri wa elimu sayansi na teknolojia , mbunge wa Nyasa Mheshimiwa Stella Manyanya, akitoa nasaa katia sherehe hizo za jubilei ya mapadre hao 11 ameitaka jamii kuwaendeleza watoto katika suala la elimu ili kupata taifa lenye watu wanaokubalika katika jamii yoyote.
Amesema “elimu inasaidia kumtengeneza mtu ili aweze kufanya kazi kadiri ya wito alionao kwa kuisaidia jamii  na hatimaye kuleta maendeleo yanayokusudiwa.”
Mapadri waliofanya jubilee zao za miaka 25 ya upadri mwaka huu katika jimbo katoliki la Mbinga ni Padri Aidan Nchimbi, Padri Amon Nchimbi, Padri Alfred Komba, Padri Bosco Ndiu, Padri Christopher Mapunda, Padri Filbeth Mbunda, Padri Joakim Lipanga, Padri Kallo Komba, Padri Mendrad Nyandindi, Padri Timoth Ndunguru na Padri Thadei Kinyero.
 Sister Tuzo Nyoni, Mbinga
 


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU