Wakristo wasilisome neno la Mungu kwa mazoea- Padri asisitiza
Waamini wametakiwa kulisoma, kulisikiliza na kuliishi Neno la
Mungu linaloongoza Maisha ya kila mwanadamu.
Hayo yamesemwa huvi karibuni na Priori Msimamizi wa Abasia ya
Peramiho Padri Silvanus Kassy OSB,
wakati akihubiri katika misa ya maziko ya sista Miriam Mbawala OSB,
iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Agenes Chipole Jimbo Kuu Katoliki
Songea.
Padri Kessy amesema kuwa, waamini waache tabia ya kulisoma na
kulisikiliza Neno la Mungu, kwa mazoea bali walitafakari na kulielewa ili
lilete mabadiliko katika maisha ya kila mmoja wetu.
Aidha amesema neno la Mungu linapotuambia tubuni na kiamini
Injili, linatutaka kila mtu binafsi kutubu, kufanya toba na kuiamini Injili na
kuamini kabisa uwepo wa Mungu na neno lake.
Amefafanua kuwa, neno la Mungu linatuambia tupendane,
tuheshimiane, tusaidiane,tusameheane, tutiane moyo na kufarijiana katika
matatizo, hivyo linatudai kulifanyia kazi katika maisha na neno hilo lilete
mabadiliko katika kila Nyanja ya maisha.
Padre Kessy amesema kuwa, tunapofanya maziko ya sista Miriam
tunadaiwa kuliishi neno la Mungu na kuwa na Imani na Mungu.
Amesema sisi sote ni
wapita njia katika dunia hii na kwamba hatutaweza kamwe kumwendea Mungu pasipo
kupitia kifo, kwani hata Bwana wetu Yesu Kristu kabla ya kuingia katika utukufu
alionja mauti.
Hivyo amewataka kujiandaa kikipokea kifo na sio kikikimbia.
“ Baadhi yetu tumekuwa tunakikimbia kifo wakati mwingine kwa
kutumia hata njia haramu ili tusife kama kwenda kupata mazindiko, kwenda kwa
waganga ili watugange. Hayo hayasaidii,” amesema.
Aidha amesema neno la Mungu linasisitiza daima waamini
wakeshe kwa sababu hatujui siku wala saa ya kifo chetu.
Akizungumzia wasifu wa sista Miriam aliyefariki akiwa na umri wa miaka 94 ya
kuzaliwa na miaka 71 ya maisha ya nadhiri za kitawa Padri Kessy amesema sista
Miriam alikuwa mtu aliyeishi kadiri ya wito wake wa utawa, alikuwa thabiti
katika wito wake, mwenye mapendo kwa Mungu na jumuiya yake,na mwenye mapendo ya
pekee kwa watoto.
Pia sista Miriam
alikuwa mtu mwenye huruma, mkarimu, mvumilivu, mwenye bidii katika utume wake
na mtu wa sala.
Akitoa neno la shukrani mama mkuu wa shirika la masista Wabenediktini
wa Mtakatifu Agens Chipole Sista Maria Asante Goliama OSB, amesema,
anawashukuru viongozi wote wa Kanisa kwa masakramenti na malezi yaliyofanikisha
sista Miriam kuwa mtawa aliyeishi kifadhila.
Sista Asante amewashukuru pia masista wa Tutzing Peramiho
waliokuwa walezi wa kwanza wa shirika la Mtakatifu Agens Chipole hadi
lilipoweza kujiongoza lenyewe.
Amesema marehemu sista Miriam ni kati ya masista wa kwanza
walioanzia maisha yao Peramiho na kuja kuanzisha makao mapya Chipole ambapo
hadi sasa wamebaki masista watatu tu waliotoka Peramiho.
Water Hack Burns 2 lb of Fat OVERNIGHT
ReplyDeleteMore than 160 000 women and men are hacking their diet with a easy and secret "liquid hack" to drop 2 lbs every night as they sleep.
It is very simple and works with everybody.
You can do it yourself by following these easy steps:
1) Go get a clear glass and fill it up half glass
2) Then follow this crazy HACK
and you'll be 2 lbs lighter the next day!