Uzinduzi wa hospitali ya saratani Ifakara


‘Msiogope kupeleka ujumbe wa Mungu kwa waliopotoka’ Ask. Libena

WAKATI Jimbo Katoliki Ifakara likiweka historia kwa kuzindua hospitali ya Saratani ya Msamaria Mwema itakayohudumia wagonjwa wa saratani nchini, Askofu wa Jimbo Katoliki Ifakara Mhashamu Salutaris Libena ametoa rai kwa watawa kuendelea kutangaza nia za Mungu kwa kupeleka ujumbe wa Mungu kwa wanaopotoka.
Rai hiyo ameitoa hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa hospitali hiyo iliyojengwa na inayoendeshwa na wamisionari wa huruma (Missionaries of Compassion), uzinduzi uliofanyika katika hospitali hiyo ambapo wananchi wa Ifakara wameshuhudia kubarikiwa kwa majengo ya hospitali hiyo ikiwa ni ishara ya kuanza utoaji wa huduma.
“Tutangaze nia za Mungu kwa kupeleka ujumbe wa Mungu kwa wanaopotoka. Wakitusikia Mungu atawapa msamaha, wasipotusikia Mungu atawapa namna nyingine ya kumsikiliza” ameeleza Askofu Libena.
Aidha katika uzinduzi huo ulioenda sambamba na maadhimisho ya sikukuu ya watawa, Askofu Libena amewakumbusha watawa nchini kushika Injili kama kanuni yao kuu huku wakijikatalia mambo ya ulimwengu na wakiunganisha sala zao na utume wanaoufanya.
“Watawa wapo katika dunia hii lakini  wanatakiwa kujikatalia mambo ya ulimwengu. Kusafiri pamoja na Kristo haina maana hakuna dhoruba itakayowapiga, bali kusafiri na Kristo ni hakika kuwa dhoruba haitashinda” amesema.
Wito kwa Serikali
Wakati huo huo Askofu Libena ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya kwa kukubali kuisajili hospitali hiyo na kutoa leseni ya kutoa huduma kwa wananchi, huku akitoa rai kwa serikali kufikiria kutoa ruzuku ili kuwezesha utoaji huduma kwa wanachi wengi zaidi.
“Tunaiomba serikali ifikirie kutoa ruzuku kwa kuwa watakaopatiwa matibabu katika hospitali hii ni watanzania wale wale” ameeleza.
Aidha amewaomba wananchi wa Ifakara waipokee hospitali hiyo kwa kuwa ni yao ambayo itarahisisha upatikanaji huduma kwa wananchi huku uchunguzi wa magonjwa utafanyika bila malipo. “Tuipokee hospitali hii kwa furaha, ni yetu, tuithamini, tutibiwe hapa”.
Akielezea upendo wa ajabu wa wamisionari hao wa huruma kwa uwekezaji mkubwa walioufanya katika kujenga hospitali Askofu wa Jimbo Katoliki Mahenge Mhashamu Agapiti Ndorobo amesema kuwa mwanzilishi wa hospitali hiyo Padri Jose Kaimlet alikuwa na maono ya kuona mbali ambayo hatimaye yamekuwa faraja kwa jamiii nzima.
“Uwepo wetu ni faraja kwa wahitaji na wenye shida mbalimbali na hii ndio maana halisi ya uwepo wa hospitali hii” amesema Askofu Ndorobo.
Katika hatua nyingine Askofu Libena ametoa rai wa wauguzi kutumia taaluma yao katika kuhudumia wagonjwa huku wakitambua kuwa wanao wajibu wa kutoa huduma ya upendo kwa wagonjwa na hivyo kuweza kumponya mtu kabla ya kutibu ugonjwa.
Ametoa rai hiyo wakati wa mahafali ya Chuo cha Uuguzi cha Edgar Maranta Kilichopo Ifakara, kinachoendeshwa na kumilikiwa na Jimbo Katoliki la Ifakara, ambapo amewaasa wahitimu hao kwenda kudhihirisha mafunzo waliyoyapata chuoni hapo ambapo tunu za maadili na utu zinasisitizwa katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa.

“Mnapotoa huduma kwa wagonjwa hakikisheni mnamtibu mtu kwanza kabla ya kutibu ugonjwa. Huduma inayoenda sambamba na upendo, utu, kuzingatia maadili na tunu mbalimbali itawafanya muweze kuwaponya watu na magonjwa yao. Nendeni mkawe bendera na kielelezo cha elimu bora mliyoipata hapa Edgar Maranta” amesema Askofu Libena.

Comments

  1. Did you realize there's a 12 word phrase you can communicate to your man... that will trigger deep feelings of love and instinctual attractiveness for you buried within his heart?

    That's because hidden in these 12 words is a "secret signal" that triggers a man's instinct to love, cherish and look after you with his entire heart...

    ====> 12 Words That Fuel A Man's Desire Impulse

    This instinct is so built-in to a man's brain that it will drive him to work harder than ever before to do his best at looking after your relationship.

    Matter of fact, fueling this dominant instinct is so binding to achieving the best possible relationship with your man that once you send your man one of these "Secret Signals"...

    ...You will soon notice him open his soul and heart for you in such a way he's never experienced before and he will recognize you as the only woman in the world who has ever truly attracted him.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI