CCBRT yazidi kuwatia moyo wenye fistula


LICHA ya uhamasishaji unaofanywa na Shirika  lisilo la Kiserikali linaloshughulika na masuala ya afya la CCBRT,kuwahamasiha  akinamama wenye tatizo la kutoka haja ndogo  au kubwa  bila kujitambua (Fistula)kujitokeza kupata matibabu bure ya ugonjwa huo, idadi inayojitokeza ni ndogo ikilinganishwa na hali halisi.
Afisa Uhusiano wa CCBRT  Bw. Abdul Kajumulo ameyasema hayo mwanzoni mwa juma wakati akizungumza na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kusimamiwa na Kanisa Katoliki nchini,mazungumuzo yaliyofanyika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) jijini Dar es Salaam.
Amesema  takribani watu 3,000 nchini Tanzania hukabiliwa na ugonjwa wa fistula kila mwaka, lakini kati ya hao ni wagonjwa 1,500 - 2,000 wanafika hospitali kwa ajili ya kupata tiba huku idadi iliyosalia wakiendelea kujificha majumbani, jambo lililoelezewa   kukwamisha juhudi za kupunguza  kasi ya zatizo hilo.
Amezitaja  baadhi ya sababu zinazochangia watu kutokupata matibabu kuwa ni pamoja na imani potofu ambapo baadhi yao wanaamini kuwa, ugonjwa huo unatokana  na kulogwa au laania.
Hivyo baadhi wanatumia mitishamba kuwatibu wagonjwa hao.
Hata hivyo amewatoa wasiwasi kuwa ugonjwa huo wa fistula siyo laana kama wengi wanavyofikiri, bali unatokana na sababu mbalimbali ikiwemo uzazi pingamizi, upasuaji, uwepo wa uvimbe kwenye nyonga pamoja na uwepo wa majeraha ya magonjwa  ya kuambukizwa na kwamba matibabu sahihi yanapatikana hospitali ambapo mgonjwa hufanyiwa upasuaji.
“Tunazidi kusisitiza kwamba fistula haitokani na kulogwa. Ni ugonjwa unaowapata akinamama kutokana na sababu malimbali na matibabu yake yanapatikana CCBRT  Dar es Salaam, huku hospitali za Kivulini Arusha, Bugando jijini Mwanza na Kinga Tabora zikitibu fistula ya uzazi na matibabu yake ni bure kuanzia gharama ya nauli ya mgonjwa,chakula,malazi na matibabu,” amesisitiza.
Bw.Kajumulo ambaye ametoa ufafanuzi huo kwa niaba ya Daktari Bingwa wa Akinamama na Mtaalam wa Upasuaji CCBRT, Dk. James  Chapa, amesema akinamama wengi wanakabiliwa na fistula ya uzazi ambalo ni tundu lisilo la kawaida linalotokea kati ya kibofu cha mkojo na uke au njia ya haja kubwa  na uke au vyote kwa pamoja , hivyo kusababisha kutokwa na haja kubwa au ndongo au vyote kwa pamoja kupitia ukeni bila kuwa na uwezo wa kujizuia..
Anatoa rai kwa mama mjamzito kuhakikisha anapata huduma ya hospitali haraka pindi anapojisikia uchungu wa kujifungua ili kuepuka na changamoto ya uzazi pingamizi inayosababisha fistula na kwamba ikitokea mtu akapata tatizo hilo la fistula ambalo moja ya dalili zake ni kushindwa kuzuia mkojo au haja kubwa, achukue hatua za kumwona daktari kwa uchunguzi zaidi ambapo matibabu yake huchukua wastani wa wiki mbili.
Hata hivyo amesema  huenda tatizo hili likapata suluhisho kufuatia CCBRT kuingia kwenye Makubaliano na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ili kuhamasisha jamii kujitokeza kutibu magonjwa mbalimbali ukiwemo fistula, miguu ya kupinda kwa watoto na midomo wazi ama midomo sungura.
Makubaliano haya yamekuja baada ya CCBRT kujiridhisha kuwa TEC ina mfumo imara unaofanyakazi kuanzia ngazi ya Taifa hadi kwenye ngazi  za chini na pia ina rasilimali zikiwemo hosptali na vyombo vya habari, vitu ambavyo vikitumika vitapunguza tatizo hili.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala  TEC, Bw. Erick Mwelulila amesema TEC kwa kutumia mifumo yake ambayo ipo kuanzia  Taifa, Jimbo, Parokia, vigango, jumuiya ndogondogo na familia na kwa kutumia rasilimali zake vikiwemo makanisa, vyombo vya habari,hospitali na shule,itafanya uhamasishaji na uelimishaji wa kina  juu ya suala hili.
“Pia viongozi wetu wa kiroho wakiwemo maaskofu na mapadri watatumia majukwaa yao ikiwemo mimbari, kufanya ushawishi kwa wanajamii kujitokeza kutibu vyote fistula, midomo wazi na miguu iliyopinda…pia baadhi ya hospitali zetu zitatumika kutoa huduma ya matibababu.

Mkataba huo baina ya TEC na CCBRT ni wa miaka mitano na umenza kutekelezwa rasmi 2019 kwa pande zote kusainiana Makubaliano ya utekelezaji  (MoU).

Comments

  1. Your Affiliate Profit Machine is waiting -

    And making money online using it is as easy as 1---2---3!

    This is how it works...

    STEP 1. Tell the system which affiliate products the system will push
    STEP 2. Add PUSH BUTTON traffic (it LITERALLY takes JUST 2 minutes)
    STEP 3. See how the system explode your list and sell your affiliate products on it's own!

    Are you ready to start making money?

    Click here to activate the system

    ReplyDelete
  2. 1xbet korean | legalbet.co.kr
    › legalbet-korean หาเงินออนไลน์ › legalbet-korean A professional poker player from Malaysia has come to 1xbet Malaysia to play some live games online in one place, with no sign 인카지노 of problem.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI