Taasisi zatakiwa kuwa na Sera ya Walemavu
Na Dalphina
Rubyema
ILI kujenga jamii yenye
usawa na kujali makundi yote, taasisi na
mashirika mbalimbali nchini yakiwemo ya kidini , yameshauriwa kutunga Sera
yenye kuwalinda na kuwatetea watu
wenye ulemavu.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa
Kitengo cha Ujumuishaji wa Watu wenye Ulemavu katika Masuala ya
Maendeleo cha CCBRT, Bw. Frederick
Msigala, wakati akizungumza na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Kuendeshwa
na Kanisa Katoliki nchini.
Katika mazungumzo hayo
yaliyofanyika katika ofisi za Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)
zilizopo Kurasini jijini Dar es Salaam, Bw. Msigala amesema licha ya asilimia
9.3 ya Watanzania kutajwa kuwa ni watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali, bado jamii
haijalipa umuhimu unaotakiwa kundi hili, jambo linalorudisha nyuma juhudi za
serikali na wadau wengine wa maendeleo.
Aliyataja baadhi ya mambo yanayokwamisha juhudi hizi kuwa ni
pamoja na baadhi ya taasisi na mashirika mbalimbali nchini kutokuwa na Sera ya Walemavu
jambo ambalo amesema linawanyima stahiki
zao.
“Ni kutokuwa na Sera ya Walemavu ndiko kunakosababisha hata
miundombinu ya baadhi ya taasisi
kutokuzingatia mahitaji ya walemavu.
Unakuta taasisi ina
kumbi nzuri za mikutano lakini ujenzi wake ni wa ghorofa na hakuna lifti kwa
ajili ya watu wenye ulemevu… vivyo hivyo mazingira unakuta yana barabara zenye
ngazi ,lakini hakuna ngazi mbetuko maalum kwa kundi hili. Hata sehemu za
kujisitiri si rafiki kwa walemavu,” amesema.
Hata hivyo amesisitiza kuwa, Sera hiyo ilinde makundi yote ya
walemavu wakiwemo wale wa viongo,
kutokuona, ngozi, viziwi na wale wenye
upoozi wa ubongo.
Bw.Msigala ambaye ni mlemavu wa viungo amesema, kutokulijali
kundi la walemavu ndiko kunakosababisha
kundi hili kuendelea kunyanyapaliwa huku baadhi ya watu wakiwachukulia kama watu wanaohitaji hisani jambo ambalo siyo sahihi.
“Ulemavu si dhambi wala laana! Si kundi linalotakiwa kutengwa
na jamii, badala yake tunatakiwa kuwawezesha kwa kuangalia mahitaji yao ya
msingi ikiwemo elimu na miundombinu rafiki ya kupata elimu hii..
Tunauwezo wa kupambanua
mambo kama ilivyo kwa binadamu wengine wasiyo walemavu , tatizo ni kwamba
hatupewi kipaumbele…hatupelekwi shule badala yaketunafichwa majumbani, na hili
linachangia sana idadi ya watu wenye ulemavu wasiyojua kusoma na kuandika kuwa
kubwa ikilinganishwa na wale watu wa kawaida,” amesema.
Kitakwimu alisema kwamba, asilimia 45 ya Watu wenye ulemavu
nchini Tanzania,hawajui kusoma na kuandika na katika watoto 10 wenye ulemavu,
wanne kati yao hawaendi shule na chini ya asilimia tano ndiyo walioajiriwa
katika sekta rasmi.
“Tusichukuliwe kama
watu wakupewa hisani… sisi ni binadamu kamili. Tuna akili na uwezo wa kupembua
mambo hata darasani tunafanya
vizuri…mfano ni kwangu mimi ambaye wazazi wangu hawakuniona mzigo tangu
awali, walinisomesha.
“Sekondari nilisoma Tosamaganga Iringa, Digrii yangu ya kwanza nilisoma Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam na Masters nimesoma Uingereza… ninauwezo ndiyo maana hata
CCBRT wameniajiri na ajira yangu siyo ya upendeleo ni stahiki yangu, hivyo
tusiwadharau watu wenye ulemavu bali tuwawezeshe kulingana na mahitaji yao,” amesisitiza.
Amesema kuwawezesha
huku kusiwe kule kwa kuwajengea nyumba au kuwatengea makazi maalum,
badala yake wapewe elimu, wawezeshwe
kupata taarifa kila kundi kulingana na mahitaji yake ikiwa ni pamoja na
kuwekewa wataalam wa alama, maandishi kuwa katika mfumo wa nukta nundu na mahitaji mengineyo.
“Kutujengea nyumba au
kututafutia makazi maalum ni zaidi ya kututenga sisi watu wenye ulemavu … ni
sawa na kutuambia tujitenge na jamii tuishi peke yetu …inasahau kwamba tunayo haki ya kuishi na ndugu,jamaa
na familia zetu kwa ujumla…hili nalo liangaliwe kwa mapana linatuumiza,” amesisitiza Bw.Msigala.
Amesema yote haya
yataondoka endapo serikali, wadau na jamii kwa ujumla itatengeneza mazingira
rafiki ya kuwawezesha watu hawa wenye ulemavu.
If you're trying hard to lose kilograms then you absolutely have to get on this brand new custom keto meal plan.
ReplyDeleteTo create this keto diet service, licensed nutritionists, fitness trainers, and cooks have joined together to develop keto meal plans that are useful, convenient, economically-efficient, and fun.
From their first launch in January 2019, hundreds of clients have already remodeled their body and health with the benefits a great keto meal plan can provide.
Speaking of benefits: clicking this link, you'll discover 8 scientifically-certified ones given by the keto meal plan.