‘Tumieni mali zenu kuwasaidia masikini’
Jimmy Mahundi, Mtwara
Waamini wametakiwa kutumia mali,utajiri na karama
mbalimbali walizojaliwa na Mungu kuutafuta ufalme wa Mungu kwa kuwasaidia
wahitaji badala ya kuzitumia kwa maslahi
binafsi.
Hayo
yamesemwa hivi karibuni na Abate wa Abasia ya Ndanda Prasidus Mtunguja OSB,wakati
wa homilia ya jumapili ya 26 ya mwaka c wa Kanisa iliyofanyika katika Kanisa la
Watakatifu Petro na Paulo jimboni Mtwara.
Ameitaka
jamii ya waamini kutumia mali zao kwa kuwakumbuka wahitaji na maskini katika
maeneo yanayowazunguka.
Abate Mtunguja
amesema kuwa Mungu amewajalia watu mbalimbali
vipawa na mali ambazo wengi wanatumia wao pekee pasipo kuwaangalia wenye shida
katika maeneo yao.
Hali hiyo
inasababisha maskini kuendelea kuteseka na kukosa huduma msingi za binadamu.
nafasi na
kwa kufanya hivyo mali haiwasaidii kuuikia ufalme wa mbingu.
“Ni muhimu
na wajibu kwa kila mmoja kuwasaidia katika mahitaji yao ikiwa ni pamoja na
ushauri,elimu na vitu mbalimbali.Hiyo ni njia mojawapo wa kujitafutia Ufalme wa
Mungu,” amesema.
Aidha amedai
kuwa, kuwa na mali au fedha sio tatizo, bali ni kuona vitu mtu alivyojaliwa
na Mungu anavitumiaje katika kujiwekea
akiba ya kweli Mbinguni.
Pia
amebainisha lipo tatizo kubwa na sugu kwa watu wengi katika jamii ya sasa kuwa
na tabia ya uchoyo na kukosa huruma ka wahitaji na wenye shida,amesema hali hii
ni hatari sana na kwa kufanya hivyo ni kukosa shukrani kwa Mungu.
Hata hivyo
amesema kuwa, matajiri wengi hawalaumiwi kwa kwa kuwa na mali bali uchoyo wao
wa kuangalia wahitaji bila kujua kuwa, kusaidia wahitaji ni kuiishi Injili na
huo ndio uinjilishaji wa kweli.
Comments
Post a Comment