Metropolitani ya Tabora yazindua Kongamano la Ekaristi Takatifu
Askofu Mkuu Paul Ruzoka wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora akiwa ndani
ya kanisa Kuu la Mtakatifu Terezia wa Mtoto Yesu Yesu Tabora.
|
Na. Thomas Mambo
-Tabora.
Majimbo yanayounda Kanda ya Magharibi (Metropolitani ya
Tabora) hivi karibuni imefanya uzinduzi wa Kongamano la Ekaristi Takatikafu
katika Makao Makuu ya Kandahiyo katika
Jimbo Kuu Katoliki Tabora ikiongozwa na kauli mbiu “Ekaristi Takatifu , Chemchemi
ya Uzima Wetu.”
Misa hiyo ya uzinduzi iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo
Kuu Katoliki Tabora Mhashamu Paul Ruzoka
imefanyika hivi karibuni katika Kanisa
Kuu la Mtakatifu Terezia wa Mtoto Yesu jimboni Tabora.
Askofu Ruzoka amesisitiza umuhimu wa kutumia mali na majaliwa
ambayo Mungu anampatia kila mmoja ili
yamsaidie katika maisha yake ya hapa duniani na baadaye katika uzima wa milele.
Aidha amesema kuwa katika ulimwengu wa sasa mwanadamu
anaweza kutekwa nyara na mali za dunia hii akasahau kuona na kujali shida ya
jirani yake.
“Kupata mali ni jambo nzuri na halina shida yoyote kwa
mwanadamu bali zitumike kwa maandeleo ya mwanadamu kiroho na kimwili.
Ni vyema kujiwekea
hazina mbinguni ili baada ya maisha haya
zitufae pia katika maisha baada ya kifo.
Kila mmoja wetu aone kuwa katika kila mwanadamu kuna sura ya Mungu.
Kwamba kila unalofanya unamfanyia Kristo mwenyewe.
Tunaweza kusoma haya
yote katika Injili ya Mathayo 25:31-46, tukifanya hayo yote basi tunakuwa
tumeanza safari ya kwenda mbinguni, safari ambayo tunapaswa kuifanya kila siku
kila mmoja wetu kwa kadri ya wito wake,” amesema.
Katika Adhimisho hilo la Misa Takatifu ya ufunguzi wa
Kongamano hilo, Askofu Ruzoka amesema Kongamano la kwanza lilifanyika huko
Ufaransa na Kongamano lijalo la mwaka 2020 katika Jimbo Kuu Katoliki Tabora
litakuwa la 52.
Katika Tanzania, Kongamano lijalo litakuwa Kongamano la nne baada
ya lile lililofanyika Dodoma, Iringa na
Mwanza .
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wajumbe kutoka Jimbo Katoliki Kigoma, Jimbo Katoliki Mpanda, Jimbo Katoliki
Kahama , Jimbo Kuu Katoliki Tabora na Jimbo Katoliki Singida.
Aidha Askofu Ruzoka
amesema makongamano haya ni fursa ni shule ya kujitathmini wapi pamelegea ili
paimarishwe na wapi pako vizuri basi padumishwe zaidi.
Kilele cha Kongamano
la Ekaristi Takatifu kinatarajiwa kuwa mwakani(2020) kuanzia Julai 1-5 mwaka 2020
katika Jimbo Kuu Katoliki Tabora na litahudhuriwa na wa kristo kutoka majimbo yote
katoliki ndani ya Tanzania na baadhi ya wageni kutoka nje ya Tanzania.
Comments
Post a Comment