Serikali yapokea ripoti ya utafiti wa viongozi wa dini kuhusu afya
Serikali yapokea ripoti ya Viongozi wa dini kuhusu hifadhi ya jamii kwenye sekta
ya afya Octoba 4 mwaka huu katika Mkutano wa Viongozi wa dini mbalimbali
uliofanyika katika Ukumbi wa Mt. Gaspari Dodoma.
Akipokea Ripoti hiyo kwa niaba ya serikali Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii
Dokta John Jingu amebainisha kuwa jukumu kubwa la serikali ya awamu ya tano
chini ya Rais Dokta John Pombe Magufuli ni kuhakikisha kuwa msisitizo mkubwa ni
kuwahudumia walio wanyonge.
Amesema kuwa viongozi wa dini wamekuwa wakihubiria waamini wao juu ya
huduma kwa wanyonge na maskini zaidi pamoja na kuwasaidia walio wadogo.
“Serikali yetu tangu ipate uhuru imekuwa ikisisitiza hivyo wakati
iliposisitiza kupiga vita maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini
ilikuwa inamaanisha hivyo” aliongeza Dokta Jingu.
Hata hivyo amesema kauli ya Rais Magufuli ya kuwa yeye ni Rais wa
wanyonge ina maana kuwa serikali yake ni ya wanyonge hivyo mkazo ni kuwahudumia
wanyonge ndio maana serikali imeweka idara maalumu ya kuwashughulikia walio
wanyonge ambayo Wizara yake ni Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee
na Watoto.
Dokta Jingu amesema kuwa Wizara yake kupitia sera yaTaifa ya Afya ya mwaka 2007 na sera ya Afya ya Wazee
ya mwaka 2003 imeweka mkazo katika
kuwahudumia walio wanyonge na hususani Wazee ambao wana umri kuanzia miaka 60
na kuendelea kupatiwa matibabu bure bila ya malipo.
Amesema kuwa katika kutekeleza sera na miongozo mbalimbali ambayo
wamekuwa wakipata katika kuhudumia makundi hayo madogo wamekuwa na ushirikiano
na tamisemi katika kuona ni namna gani ambayo wanaweza kutekeleza sera hiyo
lakini pia na idara ya kuboresha afya ya ustawi wa jamii.
Amesema katika kuhakikisha hayo wamefanya zoezi la kutambua wazee katika
halmashauri zote nchini na kuwapatia vitambulisho vya matibabu bila ya malipo
ambapo hadi kkufikia septemba 2018 wamegundua uwepo wa wazee milioni moja laki
nane na hamsini elfu na mia sita na ishirini na mbili huku wanaume wakiwa ni
laki nane nane na arobaini na saba elfu mia tisa hamsini na tano na wanawake
wakiwa ni milioni moja na elfu mbili mia sita sabini na saba wametambuliwa na
kati yao laki saba hamsini na nne elfu mia sita sitini na saba wamepatiwa
vitambulisho vya matibabu bila malipo.
Aidha Dokta Jingu amesema kuwa serikali inaendelea kuhakikisha kuwa
wazee wote ambao hawana uwezo wanapatiwa matibabu hayo lakini kumekuwapo na
changamoto katika eneo hilo ambapo baadhi ya watoa huduma wamekuwa
wakiwanyanyapaawazee hao na kwa kuliona
hilo siku ya wazeenduniani kwa hapa nchini Tanzania ilivyoadhimishwa Kitaifa
Mkoani Arusha Oktoba Mosi mwaka huu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,
Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu alitoa maelekezo na maagizo kwa wale
wote ambao wanawanyanyapaa wazee washughulikiwe.
Amesema kuwa wao kama Viongozi wameahidi kulishughulikia suala hilo na kwamba endapo mzee yeyote
atakayenyanyapailiwa katika kituo chochote kile cha afya au hospitali anapaswa
kubainisha jina la mhusika wa kitendo hicho na atoe taarifa mahali husika na
wizara itachukua hatua stahiki.
Dokta Jingu amebainisha kuwa wizara kupitia NHIF na CHIF wamekuwa
wakijitahidi kuboresha huduma za afya kwa watu wote.
“Hapa kuna changamoto kubwa ambapo kuna watu wanauwezo wa kupata huduma
hizi lakini kwa njia moja ama nyingine wanakwepa ama hawajui umuhimu wa
kujiunga na huduma hizo” aliongeza Dokta Jingu.
Hata hivyo amewaomba viongozi wa dini waliohudhuria uzinduzi wa ripoti
hiyo kuendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na mifuko inayotoa huduma za
matibabu.
“Wakati NHIF inaanza baadhi ya watu waliona kuwa mfuko huo umelenga
kuwachukulia wananchi fedha zao kumbe sio hivyo ndio maana tuliwaita watendaji
na kuwaweka kitimoto lakini baada ya kupata vitambulisho hivyo na kuanza kutoa
huduma faida imeonekana lakini kuna haja ya kufanya ulazima wa kuhakikisha kuwa
kila mfanyakazi wa serikali anajiunga na mfuko huo wa NHIF” aliongeza.
Dokta Jingu amesema kuwa kwa sasa inabidi kuwepo na kulazimisha watu
kujiunga na NHIF kwani wengi wanakuwa wakipinga bila ya kujua wanachopinga na
baadae wanapogundua faida zake wanajilaumu.
Dokta Jingu amesema lengo la utafiti na mapendekezo yanayotoakana na
utafiti sio kutoa mahitimisho isipokuwa ni kuchocvhea fikra ili tuzidi kufikiri
zaidi na kushughulikia changamoto zilizopo.
Ripoti ya viongozi wa dini kuhusu hifadhi ya jamii kwenyesekta ya afya.
Akiwasilisha Ripoti hiyo ya
Viongozi wa dini Mtafiti katika Kamati ya Dini mbalimbali nchini Dr.nMoses
Kulaba amesema kuwa, ripoti hiyo inajaribu kujibu swali, ‘ Tunaweza je kuongeza
upatikanaji wa hifadhi ya jamii kwenye sekta ya Afya kwa kutumia mapato au
fedha mapato ya ndani?
Amesema ripoti inaonyesha
Tanzania inaweza kuongeza au kugharimia
upatikanaji wa Bima ya Afya kwa Watanzania wote (Universal Health
Coverage) kwa kutumia fedha za mapato yake ya ndani (Own tax sources) bila
kutegemea ufadhili mkubwa kutoka nje.
Ripoti imetazama hali ya sasa hivi ya upatikanaji wa Bima ya Afya kwa
watanzania na haswa watu wa kipato cha chini
Imeangalia mafanikio na mapungufu ya kisera , ki takwimu na
kibajeti na changamoto za upatikanaji wa
bima ya Afya kwa watanzania.
Inaendelea Uk. 8
Inatoka Uk. 4
Ripoti inapendekeza njia mbadala za muda mfupi na mrefu zinazoweza kusaidia Serikali kugarimia watu
au kaaya masikini wapate bima Afya na
kuongeza usajili wa idadi ya watu wenye Bima ya Afya kutoka asilimia 32 mpaka
Asilimia 100 ifikapo 2025.
Tarifa zinaonyesha changamoto kubwa za kisera , ki mfumo na kifedha za
upatikanaji wa bima ya Afya
Wakati wa kukusanya tarifa takwimu kutoka serikali zilionyesha kati ya
hawa asilimia 32 asilimia 7- 8%
wamejiunga na Bima ya Afya au
(National Health Insurance Fund -NHIF), 23%
wamejiunga na Mfuko wa Bima ya Jamii ( Community Health Fund -CHF). Na asilima
moja wamejiunga na Makampuni binafsi ya kutoa Bima za Afya. (National
Health Insurance Funds (2017) Annual fact sheet 2016/2017, NHIF Dar es Salaam).
Tafsiri yake ni kwamba asilima 68 ya Watanzania wote hawana Bima ya
Afya. Wakipata matatizo ya Afya wanalazimika kuingia mifukoni kulipia garama za
huduma ya Afya.
Kati ya hawa asilimia 68 kuna asimila 40 wanaweza kuchangia malipo ya
bima ya Afya lakini kuna asilimia 28 takribani ya watu kam 14.3 million ni masikini sana na hawana uwezo kulipia bima
ya Afya
Tafsiri yake ni kwamba bila msada
hawa wakipata matatizo ya Afya wanaweza kukosa matibabu na pengine hadi
kufa.
Kwa kufanya mabadiliko madogo madogo sana kwenye sera za kodi mbali
mbali serikali inaweza kabisa kupata pesa ya kulipia hawa asilimia 28 masikini
na kutenga pesa za kulipia (matching funds) za wale asimila 40 ambao
bado hawajajiunga.
Fedha hizi zinaweza kutokana na kuanzishwa utaratibu wa kutenga kiasi
cha fedha kutoka vyanzo mbali mbali vya kodi (ring fenced revenues) kama sekta
ya madini na vyanzo vingine bila
kuongeza kodi na kuelekeza pesa hizi kugharimia bima ya Afya.
Kwa kulenga asilimia kugarimia
asilimia 17 kila mwaka ya wananchi wote walio nje ya bima serikali inaweza kuongeza upatikanaji wa bima
kutoka asilimia 32 hadi 91 ndani ya miaka miwili na hadi asilimia 99 au 100
ifikapo 2025.
Uzoefu kutoka nchi nyingine unmeonyesha kwamba kwa kuthubutu kabisa na
thamira ya makusudi (national political
and leadership will) inawezekana.
Kuna mahusiano kati ya Afya mbaya na umasikini na kuwekeza kwenye Afya
ni mtaji (social investment) kubwa kwa nchi kwahiyo kuna haja kubwa sana ya
kuangalia jambo hili kwa uzito huo na kuwezesha upatikanaji wa bima ya Afya
haraka iwezekanavyo.
Kwa kufanya mabadiliko madogo madogo sana kwenye sera za kodi mbali
mbali serikali inaweza kabisa kupata pesa ya kulipia hawa asilimia 28 masikini
na kutenga pesa za kulipia (matching funds) za wale asimila 40 ambao
bado hawajajiunga.
Pesa hizi zinaweza kutokana na kuanzishwa utaratibu wa kutenga kiasi cha
fedha kutoka vyanzo mbali mbali vya kodi (ring fenced revenues) kama sekta ya
madini na vyanzo vingine bila kuongeza
kodi na kuelekeza pesa hizi kugharimia bima ya Afya.
Kwa kulenga asilimia kugarimia
asilimia 17 kila mwaka ya wananchi wote walio nje ya bima serikali inaweza kuongeza upatikanaji wa bima
kutoka asilimia 32 hadi 91 ndani ya miaka miwili na hadi asilimia 99 au 100
ifikapo 2025
Uzoefu kutoka nchi nyingine unmeonyesha kwamba kwa kuthubutu kabisa na
thamira ya makusudi (national political
and leadership will) inawezekana
Kuna mahusiano kati ya Afya mbaya na umasikini na kuwekeza kwenye Afya
ni mtaji (social investment) kubwa kwa nchi kwahiyo kuna haja kubwa sana ya
kuangalia jambo hili kwa uzito huo na kuwezesha upatikanaji wa bima ya Afya
haraka iwezekanavyo
Kiasi gani cha fedha kinahitajika na kitoke wapi?
Dr. Kulaba amebainisha kiasi kinachohitajika kugarimia asilimia 28
ya masikini wasio na bima ya afya kuwa
ni shillingi 180 kama serikali
ikiamua kulipa garama yote (elfu 60, 000) ya bima ya afya ya jamii
iliyoboreshwa (iCHF) kwa kila kaaya.
Lakini, kaaya hizo masikini wakichangia angalau elfu kumi kwa mwaka na
serikali kuongezea elfu hamsini, garama ni yote kwa miaka mitano in
billion150.
Serikali inahitaji billion 127.2 ilikulipia kama mchango wake (matching
fund) kwa wale asilimia 40 ambao wanauwezo lakini bado hawajajiunga lakini
wanaweza kuijunga wakihamasishwa.
Kumbe serikali ikitenga billion
277 leo au ndani ya miaka mitano inaweza kufikia asilimia 91 ya watanzania wote
na bima ya afya ifikapo mwaka 2025 kwa kutumua fedha za mapato ya ndani .
Serikali inahitaji billion 290 ili kuwafikia asilimia miamoja ya
watanzani wote (ikiwemo na wanolipiwa na makampuni binafsi) kupata bima ya Afya
ndani ya miaka 5-6.
Ili kupunguza mzigo wa kibajeti serikali inaweza kulenga kufikia kaaya
asimilia 17 kila mwaka kwa miaka mitano hadi sita.
Serikali inaweza kulipia kaaya
masikini (28 ya wananchi wote nchini) kwa kutenga asilimia 19 tuu kutoka kwenye
vyanzo vya kodi mbali mbali.
Kiwango cha kodi kutoka kodi ya ongezeko ya thamani ni kidogo sana sawa
na asilimia 0.15% kila mwaka na kufikia asilimia 0.9% in 2025.Viwango hivi ni
vidogo na vinawezekana .
Serikali ianzishe utaratibu wa kutenga asilimia ya kiasi kutokana na
vyanzo vya kodi mbali mbali kama tulivyopendekeza hapo juu ili kulipia garama
bima ya Afya (Health Insurance Coverage).
Serikali iwawezeshe kaaya masikini (asilimia28) kupata bima
ya afya kwa kulipia elfu 50,000 huku kaaya zikichangia elfu 10,000.
Serikali itenge pesa za kutosha kuchangia kaaya asilimia 40 ambao wako
kwenye sekta binafsi kama mchango (matching fund) wanapojiunga.
Kuna haja ya kuhamashisha wananchi wengi kujiunga na Bima za Afya..
Msistizo tuelekeze kwenye vijana
wajiunge kwa wengi.
Matatizo na changamoto za watoaji na utoaji huduma ya Afya chini ya
mipango ya Bima Afya yatatutliwe mara moja. Kwa mfano, kuchelewesha malipo,
kukosekana kwa dawa na wahudumu, nk
Kupunguza garama za uendeshaji wa mifuko ya Bima ya Afya na kuongeza
kiwango cha pesa kinachofika kwenye vituo vya Afya
Viongozi wa dini wanapendekeza kuwepo kwa mfuko rasmi (National
Sovereign Fund) ya Afya na utaratibu wa kupeleka pesa kwenye mfuko kutoka sekta
nyingine kama madini ya Oil and Gas Fund.
Aidha ripoti imetoa majukumu kwa serikali na viongozi wa dini huku
wakiitaka Serikali kufanya Mabadiliko ya kisera , kimufumo na utaratibu wa
kikodi, Upatikanaji wa huduma na malipo kwa watoa huduma.
Viongozi wa dini wafanye Uhamasishaji wa wananchi Kutoa huduma kupitia
vituo vyao vya afya Kufuatilia na tathmini ya upatikanaji wa huduma, ubora nk.
Comments
Post a Comment