Balozi wa Baba Mtakatifu afanya ziara ya kichungaji Jimboni Musoma
Balozi wa Baba Mtakatifu nchini
Askofu Mkuu Marek Solczynski amefanya
ziara ya kichungaji kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa kwake,katika Jimbo Katoliki
Musoma kuanzia Oktoba
02 hadi 09 mwaka huu.
Katika
ziara hiyo Balozi huyo ametembelea maeneo mbalimbali ambapo Oktoba 02 alikuwa
katika Parokia ya Kiabakari na aliongoza Ibada ya uzinduzi wa kituo cha Hija ya
Huruma ya Mungu Kiabakari na kukipandisha kutoka hadhi ya Kijimbo hadi hadhi ya
Kitaifa pamoja na kubariki Kikanisa (chapel)
cha Bikra Maria.
Ametembelea
kliniki ya meno na macho katika kituo cha afya cha Blessed Pier Giorgio
Frassati Kiabakari na kubariki wagonjwa.
Akiwa
Parokiani hapo alikutakutana pia na mapadri ,watawa na waamini wa udekano wa
Butiama.
Oktoba
03 Balozi huyo akiwa katika Kanisa Kuu la
Musoma alishiriki kusali Rozari Takatifu na waamini wa parokia hiyo na
aliongoza ibada ya Baraka Kuu na baadae
alikutana na watawa na waamini wa
udekano wa Musoma .
Oktoba 04 ametembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mara, baadae ameadhimisha Misa Takatifu
na katiak Seminari ndogo ya Makoko kisha kuwatembelea manovisi na
kuwabariki masisita wazee na wagonjwa
katika nyumba yao iliyopo Makoko. Pia amefanya mazungumzo na masista wa shirika
la Moyo safi wa Maria Afrika .
Oktoba 05,atatembelea Parokia ya Utegi ambapo
atabariki wakristo na kubariki jiwe la msingi la nyumba mpya ya mapadri.
Kisha
ataelekea Tarime ambapo atawabariki wakristu
na kubariki jiwe la msingi la
Kanisa jipya la parokia ya Tarime.
Oktoba 06,atatembelea Parokia ya Mugumu na
ataadhimisha Misa na kutoa Sakramenti ya ubatizo kwa watoto wachanga na kuwapa
watoto Sakramenti ya Komunyo ya kwanza
kisha atabariki nyumba mpya ya masista,baadae ataelekea Fort Ikoma Serengeti.
Oktoba
07 ,atasali Misa Takatifu katika Parokia
ndogo ya Serengeti(Fort Ikoma)kisha atakwenda Seronera.
Oktoba
8 ,atakuwa na Misa Bilila na katika Jumuiya ya Mt. Francis wa Assis na wakristo wa eneo hilo,baadae ataelekea
Serena,ambapo atasali Misa katika
Jumuiya ya Mtakatifu John Paul II.
Oktoba
09 ataondoka eneo la Serengeti na
kuelekea Mwanza .
brasliaac-ga Mary Harris link
ReplyDeletestutraffrili