MAMBO YA MSINGI KUHUSU KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 150 YA UKRISTO

Wapendwa mapadri, watawa, walei napenda kuwafikishia rasmi taarifa juu ya kilele cha maadhimisho kitaifa ya miaka 150 ya uinjilishaji Tanzania bara.

Kilele kitakuwa Bagamoyo:
·         Kuwasili Ijumaa  2.11.2018
·         Semina/sala        3.11.2018
·         Misa ya Kilele       4.11.2018

Mahali: Bagamoyo (Jimbo Katoliki la Morogoro), Mkoa wa Pwani.

Mchango wa Kila Mshiriki:
· Watu wazima ni shilingi laki moja na nusu (150,000/=).  
· Watoto ni shilingi elfu tisini (90,000/=).  

Kuhusu mchango wa ushiriki
· Mchango utumwe kwenye namba akaunti ifuatayo:

Jina la Akaunti: 150 JUBILEI KANISA KATOLIKI
Namba ya Akaunti: 00111509958201
Jina la Benki: MKOMBOZI COMMERCIAL BANK PLC
Benki Swift Code: MKCBTZTZ

· Kivuli cha listi ya malipo itumwe kwa Ndugu Erick Mwelulila (0764025761/finance@tec.or.tz) Mkurugenzi wa Fedha na Utawala TEC.
· Malipo yote yafanyike kwa njia ya benki

Utoto Mtakatifu: Tukizingatia ukweli kuwa watoto wa utoto mtakatifu wengi watashuhudia na kuadhimisha Jubilei ya Miaka 200 ya Ukristo Tanzania ni vyema wakaja kwa wingi hasa kutoka majimbo yaliyo karibu na Bagamoyo ili kuwarithisha mikoba ya uinjilishaji.

Misa siku ya Kuwasili: Tarehe 2/11/2018 itaadhimishwa misa ya kuombea marehemu wote tukiwakumbuka kwa namna ya pekee marehemu wamisionari.

Misa tarehe 3/11/2018: Misa ya Bikira Maria (Nyota ya Uinjilishaji na Msimamizi wa Tanzania)

Misa ya Kilele: Tarehe 4/11/2018 itaadhimishwa Misa kwa Ajili ya Kueneza Dini (Misa ya Uinjilishaji).
Novena: itaanza tarehe 24 Oktoba 2018 hadi 1 Novemba kuombea mafanikio ya kilele cha Maadhimisho ya Miaka 150 ya Unjilishaji Tanzania Bara, kuomba uimarishaji wa imani, moyo wa umisionari na ushuhuda wa maisha na kuiombea Tanzania amani.    

Wenu katika Kristo,
Pd. Faustin Kamugisha

Mratibu- Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania Bara

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI