Posts

Wazazi warithisheni watoto elimu-Askofu Nyaisonga asisitiza

Image
Na Thompson Mpanji, Songwe WAAMINI   wa Kanisa Katoliki   wametakiwa kuwaendeleza watoto wao katika elimu   ikiwemo na wao wenyewe kujiendeleza katika fani mbalimbali   ili waweze kujiajiri   kupitia mafunzo mbalimbali waweze kujitegemea.   Elimu ndiyo hazina pekee   na urithi mkubwa kwa familia na jamii kwa ujumla katika   maisha ya sasa   na ya baadaye. Ushauri huo umetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya,Mhashamu Gervas Nyaisonga   wakati wa homilia yake   katika adhimisho la Ibada ya Misa Takatifu   iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Francisco wa Asiz, Kigango cha Mkwajuni,Parokia ya Mwambani,jimboni humo. Walioshiriki ibada hiyo licha ya waamini wa parokia hiyo, walishiriki pia Wafanyakazi wa Hospitali ya Mwambani inayomilikiwa na Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya, iliyopo katika Kigango hicho ambako Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya Mhashamu Gervas Nyaiaonga alifanya ziara ya kutembelea H...

Askofu Ruwa’ichi: Msiabudu mali

Image
Na Dominic Haule, Dar es Salaam waamini nchini wametakiwa kuacha kuabudu mali zao kama vile biashara, mashamba, ofisi,mifugo mazao nk. badala yake   wamwabudu   Mungu pekee mtoaji wa vyote. Hayo yamesemwa na Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi   wakati   wa homilia yake   hivi karibuni katika Jubilee ya Miaka 50 ya Updri ya Padri Camille Neuray Paroko wa Parokia ya Mt.karoli Lwanga Yombo Dovya. “Kinacho tutunza sio mali, bali ni Mungu mwenyewe anaye sitawisha   mali na kuzifanya zizae. Hivyo tunapaswa kumwabudu Mungu na sio kitu kingine chochote,” amesema.   Amesema kuwa adhimisho la jubilee ni jambo linalobeba maana   kadhaa miongoni wa mambo hayo ni fursa   ya kumshukuru Mungu, kujiweka wakfu upya, kujiaminisha kwake tena kujinyenyekesha na kuomba toba   pamoja na neema na baraka. Hata hivyo Amesema kuwa watumishi wa Mungu wanatakiwa kuwa kama akina Paulo, Adrea , ...

TANZIA

Image

Baadhi ya Wakurugenzi wa fedha wa majimbo yote ya Kanisa Katoliki pamoja na Wakuu wa fedha wa taasisi za TEC walipo kutana kujadili masuala mbali mbali yahusuyo fedha (Picha na Philipo Joseph)

Image

ASKOFU MSTAAFU GABRIEL MMOLE AFARIKI

Image

TEC yawataka watunzi wa nyimbo za Kanisa kuzingatia miongozo ya Kanisa

Image
Na Dalphina Rubyema, Dar es Salaam KANISA Katoliki nchini limezidi kuwasisitiza watungaji na waimbaji wa muziki wa Kikatoliki kuzingatia misingi na miongozo ya Kanisa hilo badala kuiga mitindo na mahadhi ya   madhehebu mengine. Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Idara ya Liturujia ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Mhashamu Salutaris Libena, katika mahojiano maalum   na KIONGOZI, muda mfupi baada ya kufunga mkutano wa mwaka wa Liturujia Taifa, uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha wajumbe wa Kamati ya Muziki kutoka Kanda za Kanisa Katoliki nchini, Waratibu wa Liturujia wa Majimbo, Walimu wa Liturujia katika Seminari Kuu na baadhi ya vyuo vya Makatekista nchini. Amesema kuwa kama inavyosisitizwa kwenye Katiba ya Utume wa Kwaya Katoliki Tanzania (UKWAKATA), mtindo uimbaji ukiwemo utoaji wa sauti katika muziki Mtakatifu wa Kanisa hilo, haunabudi kuwa wa kiasili au kibantu na siyo wa kuiga mahadhi ya nje ama ya madhehebu mengine. “Waimbaji w...