Posts

Benki ya Mkombozi yafungua tawi Iringa

Image
Na Getrude Madebwe, Iringa B enki ya Biashara ya Mkombozi imefungua tawi mkoani Iringa ikiwa ni utekelezaji wa mipango ya Benki hiyo kupanua huduma zake ili kuwahudumia wananchi kwa ukaribu. Akifungua tawi hilo, Askofu wa wa Jimbo Katoliki Iringa Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa amewataka waamini wa jimbo hilo, wananchi na watu wenye mapenzi mema kuitumia Benki ya biashara ya Mkombozi ambayo imeanza kutoa huduma zake mkoani humo. Benki hiyo inatoa huduma mbalimbali za kibenki ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo kwa vikundi, mtu binafsi, taasisi na mashirika mbalimbali. Tawi hilo la Iringa ni kati ya matawi 10 ya Benki hiyo lengo ikiwa ni kuenea nchi nzima. Awali, Askofu Ngalalekumtwa ameyabariki majengo ya Benki hiyo yaliyopo kwenye Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki cha Ruaha (RUCU) na amesisitiza umuhimu wa kuweka akiba kwenye benki. “Tulitamani sana kuidhisha lile ambalo tumeidhinisha leo hii, benki ambayo tumeishughulikia sasa imefunguliwa hapa kwetu, ni nafasi ya b...

Ukeketaji, umasikini, ugomvi wa wazazi chanzo cha watoto kuzikimbia familia

Image
Na Veronica Modest Musoma U masikini , ukeketaji   na kuvunjika kwa ndoa    katika   familia kumetajwa kuwa ndio chanzo cha watoto wengi kukimbia familia zao na kujikuta wanakuwa wa mitaani. Pia hali hiyo imetajwa kuchangia watoto wengine kuzikimbia familia zao na kulelewa katika vituo vinavyowasaidia watoto   wenye mahitaji   maalum.   Hayo yamesemwa na wasichana   15 waliohitimu mafunzo ya fani mbalimbali ya stadi za maisha wa kituo cha Jipe Moyo kilichopo katika Parokia ya Mwisenge Jimboni Musoma ambao walikimbia ndoa za utotoni, Ukeketaji, waliobakwa na kufanyiwa vitendo vya ukatili na hatimaye kukimbia familia zao na kulelewa na kituo hicho kwa zaidi ya maiaka miwili.   Msimamizi wa Kituo hicho Sr Maria Annunciata Chacha amesema   kwa sasa kituo kina zaidi ya watoto 130 wanaohudumiwa na wanakabiliwa na upungufu wa chakula. Hivyo ameiomba Serikali   kuwasaidia chakula walau   hata mlo mmoja kama ni mchana ...

Viongozi wa dini watakiwa kulinusuru Taifa

Image
Na Rodrick Minja, Dodoma M WENYEKITI wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania Alhaji Ibrahim Molel amewataka viongozi wa dini kulisaidia taifa katika kuliletea maendeleo ya kiuchumi, badala ya kutofoautina na kupigana vijembe. Alhaji   Molel amewataka viongozi hao kuwa na umoja pamoja na kuvumiliana katika imani ili waweze kusonga mbele na hatimaye kuliwezesha taifa kufikia malengo yake ya uchumi wa viwanda. Mwenyekiti huyo amesema hayo   wakati alipokuwa akifungua kikao cha elimu elekezi na namna ya kuongoza katika mikoa   na wilaya na jinsi ya kueneza maridhiano   kwa kila eneo kwa   viongozi   kutoka madhehebu mbalimbali ya dini waliotoka mikoa ya Tanzania   Bara kilichofanyika jijini Dodoma hivi karibuni Amesema kuwa viongozi hao badala ya kupigana vijembe na kushindwa kusameheana watumie muda huo kwa ajili ya kujenga nchi   kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi yatakayofaidisha kila mtanzania hapa nchini. Akizungumza kwenye kikao hicho ...