Bweni lateketea, Biblia na Rozari pekee vyasalia
Mwanafunzi wa Seminari ndogo ya St. Mary Mbeya akionyesha Biblia Takatifu iliyosalimika mara baada ya moto kuteketeza vifaa vilivyokuwa katika moja ya mabweni seminarini hapo hivi karibuni (Picha zote na Thompson Mpanji) Baadhi ya vifaa vilivyoteketea kwa moto lakini Biblia na Rozali zilikutwa salama Hata baada ya moto kuteketeza vifaa hivi, Biblia na Rozari vimekutwa salama θ Ni Seminari ndogo ya St. Mary Mbeya J ANUARI 21 mwaka huu zaidi ya wanafunzi 52 wa Shule ya Seminari ndogo ya St.Mary’s ya Mbalizi Jimbo Katoliki Mbeya wamenusurika kifo kutokana na ajali ya moto ulioteketeza bweni lote na vifaa vilivyokuwemo. Aidha tukio jingine la ajabu ni kutoungua kwa Biblia na Rozali Takatifu zilizokuwa zimehifadhiwa katika masanduku ya bati ya wanafunzi licha ya vingine vyote na jengo kuteketea kwa moto. Akizungumza na Gazeti Kiongozi, Gombera wa Seminari hiyo Padri Edwin Mwimba am...