Posts

Mitandao isiwatenge na Mungu-Askofu Mstaafu awaonya vijana

MWENYEKITI wa jukwaa la Kikristo Tanzania, mkoani Mbeya, Askofu mstaafu John Mwela, amewaonya vijana wa kitanzania kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii na kukua kwa sayansi na teknolojia kusiwatenganishe na Mungu. Askofu Mwela ameyasema hayo wakati akikabidhi  misaada mbalimbali ya vyakula, nguo na mahitaji muhimu ikiwemo vifaa vya shule vilivyochangwa na wasamaria wema wa kikristo na kiislamu jijijini Mbeya na kuwasilishwa kwa Shirika lisilo la kiserikali  la Sauti ya Mama Afrika(SAMAFO) akisema kuwa mitandao ya kijamii imekuwa ikiwaondolea vijana walio wengi hofu ya Mungu na kuiga matendo yasiyompendeza Mungu. Ametoa wito kwa shirika la Sauti ya Mama Afrika kuendelea kutoa elimu  kwa jamii  hasa vijana na  familia majumbani kuwa wasimsahau Mungu kwani kwa sasa hali imekuwa ni mbaya kwa vijana walio wengi  wamefikia  hatua ya kuona kwamba Mungu yupo katika mitandao wanayoperuzi. Askofu Mwela  amesema  kwa sasa  dunia  ni kam...

‘Wanaovaa rozari bila kusali wanakufuru’

Image
θ   Wamo wasanii, waamini na wanaoning’iniza kwenye magari WAAMINI nchini wametakiwa kutumia vizuri visakramenti ikiwemo Rozari Takatifu ili waweze kuimarika kiimani. Rai hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti na Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba Mhashamu Desderius Rwoma na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Padri Raymo nd Saba, ambapo wote wamekemea tabia ya watu kuvaa rozari bila kusali. Akiongoza Misa Takatifu ya ufunguzi wa Kongamano la TYCS Kitaifa Askofu Rwoma amesema kuwa rozari siyo pambo la kuvaliwa au kuwekwa ndani, bali inamtaka muumini kuitumia kwa kusali na kuimarika kiroho. Aidha Askofu Rwoma amekemea tabia ya wasanii kuvaa rozari katika kazi zao huku matendo wanayofanya katika nyimbo zao au filamu kutoendana na uwepo wa rozari hizo. “Unakuta wasanii wanavaa rozari kwenye nyimbo zao lakini yanayotendeka humo hayafanani kabisa. Tumieni visakramenti hivi vizuri, mnaovaa rozari mkumbuke kwamba siyo pambo hilo. Rozari iwasaidie kum...

MAGAZETINI LEO IJUMAA 28 APRILI

Image

Askofu Mkuu Marek ateuliwa Balozi wa Vatikani nchini Tanzania

Image
BABA Mtakatifu Fransisko amemteua Askofu Mkuu Marek Solczyński kuwa Balozi mpya wa Vatikani nchini Tanzania. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Mkuu Solczyński alikuwa Balozi wa Vatikani nchini Georgia, Armenia na Azerbaijan. Itakumbukwa kwamba, Askofu Mkuu Solczyński alizaliwa Aprili 7, 1961 huko Stawiszyn, nchini Poland. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, mnamo Mei 28, 1987 akapewa Daraja Takatifu ya Upadri. Baada ya kufanya utume wake katika masuala ya diplomasia sehemu mbali mbali, tarehe 26 Novemba 2011, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu Mkuu na kumwekwa wakfu tarehe 6 Januari 2012. Askofu mkuu Marek Solczyński ameshiriki kikamilifu katika maandalizi ya hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Fransisko nchini Georgia, Armenia na Azerbaijan aliyoitekeleza mwaka 2016.

MAGAZETINI LEO JUMANNE APRILI 25

Image