Posts

Simanzi yatawala mazishi ya Pardi Andrew Lupondya

Image
Maaskofu wa majimbo manne , mapadri , watawa na mamia ya waamini  wameshiriki misa ya mazishi ya Padri Andrew  Lupondya (33)  na watoto watano wa  shirika rafiki wa utoto wa Yesu (VIFRA)  na mlezi wao Mama Judith  Kajwahula (63 )  wa jimbo Katoliki Kahama waliofariki  katika ajali ya gari. Ajali hiyo ilitokana na gari walilokuwemo kugongana uso kwa uso na roli aina ya fuso Disemba 24  na marehemu wamezikwa katika eneo la kiwanja cha  kanisa kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga parokia ya Kahama mjini. Misa ya mazishi  imefanyika katika kanisa kuu la jimbo na  imeongozwa na Askofu Fravian Kasala wa jimbo Katoliki Geita, pamoja  na  Maaskofu  Liberatus  Sangu wa Shinyanga, Joseph Mlola wa Kigoma  na mwenyeji Askofu Ludovick Minde wa Kahama. Akihubiri katika misa hiyo Askofu wa jimbo Katoliki Shinyanga Liberatus Sangu amesema “Kifo ni fumbo la Kristo, alishinda  maut...

Askofu Ngalalekumtwa awataka waamini kuwaombea Mapadri

Image
ASKOFU wa Jimbo Katoliki Iringa Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa amezindua mwaka wa Jubilei ya miaka 100 ya mapadri wazalendo na kuwataka waamini kuendelea kuwaombea mapadri popote walipo. Uzinduzi wa jubilei hiyo umefanyika kwenye kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu Parokia ya Kihesa kwa  kuwashwa kwa mshumaa mara baada ya Askofu Ngalalekumtwa kumaliza kutoa daraja la ushemasi kwa mafrateli Jerome Mtatifikolo wa parokia ya Ilole na Jerome Mponzi wa parokia ya Nyakipambo. Akitoa homilia kwenye misa hiyo Mhashamu Ngalalekumtwa amesema kwamba, sambamba na utoaji wa daraja hilo lakini pia waamini wanatakiwa kuwaombea viongozi wa Serikali ili waweze kutenda kazi zao kiuaminifu. Mhashamu Ngalalekumtwa amesema Kristo ndiye mfalme wa amani, kwa hiyo wanapokumbuka hayo katika historia kuuawa kwa watoto wadogo tena wasio na hatia wamuombe Kristo ili aweze kuratibu kwa wale wanaosimamia maslahi ya ulimwengu kusudi hawa watawala wawajibike ipasavyo. “Leo ni siku ya kuw...

“Shirikishaneni kumaliza maradhi ya kiroho” Askofu Mkude

Image
MOROGORO, “Moyo mlionao wa kushikana mikono na kutatua yanayowakabili mwilini kama magonjwa na kadhalika muwe na ushirikiano huo huo kutatua maradhi ya rohoni yanayowakabili.” Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Askofu  wa Jimbo Katoliki Morogoro   Mhashamu Telesphor Mkude alipokuwa akihubiri kwenye maadhimisho ya hija ya Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA) iliyoazimishwa katika parokia ya Mgeta. Askofu Mkude amesema binadamu wamekuwa wepesi kusaidiana kwenye mambo ya mwilini kama magonjwa, sherehe na mengineyo yahusuyo mwili lakini ushirikiano huo haupo kwenye kutatua magonjwa ya kiroho. “Kuna watu wanaumwa na magonjwa ya rohoni hivyo mtu anapokuja na kukueleza jambo lake msikilize kwa makini wengine misaada wanayotaka siyo ya fedha, chakula wala mavazi ila wanataka wasaidiwe kiroho na amani yao ipatikane,” amesema Askofu Mkude. Amesema mtu ambaye shida yake ni ya kiroho ni lazima itatuliwe kiroho na usikatishwe tamaa katika shida aliyonayo kwa ku...

MAGAZETINI LEO IJUMAA DEC 30

Image

USHEMASI IRINGA

Image
ASKOFU wa Jimbo Katoliki Iringa Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa amezindua mwaka wa Jubilei ya miaka 100 ya mapadri wazalendo na kuwataka waamini kuendelea kuwaombea mapadri popote walipo. Uzinduzi wa jubilei hiyo umefanyika kwenye kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu Parokia ya Kihesa kwa  kuwashwa kwa mshumaa mara baada ya Askofu Ngalalekumtwa kumaliza kutoa daraja la ushemasi kwa mafrateli Jerome Mtatifikolo wa parokia ya Ilole na Jerome Mponzi wa parokia ya Nyakipambo. Akitoa homilia kwenye misa hiyo Mhashamu Ngalalekumtwa amesema kwamba, sambamba na utoaji wa daraja hilo lakini pia waamini wanatakiwa kuwaombea viongozi wa Serikali ili waweze kutenda kazi zao kiuaminifu.