Askofu Kinyaiya awataka waamini kuwaombea viongozi wa dini
ASkofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya amewataka waamini na wote wenye mapenzi mema kuwaombea mapadri na watawa ili waweze kutimiza wajibu wao ipasavyo. Wito huo hivi karibuni kwenye Misa ya kubariki mafuta ya wagonjwa, wakatekumeni na kuweka wakfu mafuta Matakatifu ya Krisma, katika Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo Kuu Katoliki Dodoma. Askofu Kinyaiya amesema kuwa mapadri ambao ndio wapakwa mafuta matakatifu wanapaswa kutambua kuwa wao ndio wateule wa Bwana wanaofanya kazi maalumu ya kutoa huduma katika Kanisa Mahalia. ‘’Ndugu zanguni mapadri na watawa nyie ndio mliopewa jukumu la kuwahudumia wana wa Mungu katika Kanisa hivyo mnapaswa kutenda yaliyo mema na ya kuwapendeza waamini mahali. Katu msifanye kazi ya Kanisa kwa ubaguzi. Tendeni kwa haki kwa kila mmoja atakayehitaji huduma ya kiroho,” amesema Askofu Kinyaiya. Pia akizungumzia jinsi Mafuta Matakatifu ya Krisma yanavyochanganywa kuwa mafuta Matakatif...